HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)
HADITHI YA
BABA MASUMBUKO
Mtunzi: PAUL.M YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook Yahilima PM
SEHEMU YA TATU
Japo jambo hilo lilikuwa ni gumu lakini sikuwa na jinsi ya
kufanya,kwa haraka nilikiingiza kichwa cha mke wangu mkubwa kwenye ile kamba
niliyoiandaa vizuri,lakini nilipotaka kuivuta kamba ili nimninginize kwenye mti ili
ionekane kuwa amejinyonga nikiwa bado
nafikilia kufanya unyama huo,wazo likanijia kichwani kuwa tayari mke wangu
atakuwa ameshakufa kutokana na rungu niliyompiga upande wa nyuma ya kichwa,Baada
ya tukio hilo nilianza kutoka kwenye ule
msitu kwa tahadhari kubwa huku nikiangalia kama kuna mtu ameniona au la lakini nilibaini
kuwa hakuna mtu yoyote aliyeniona,nikatembea hadi nyumbani huku mapigo ya moyo
yakiwa yameongezeka na hofu kubwa moyoni ilinijaa,nilifika nyumbani nikamkuta
mke wangu mdogo akiwa mwenye furaha sana na aliponiona tu alinikimbilia.
Mume wangu! Tayari?
Tayari nini?
Umeshammaliza tayari Yule kidudu tayari?
Nilijibu kwa kutikisa kichwa na mke wangu alinipongeza huku
akiniita majina ya sifa kama kidume,simba,jabari na mengine mengi ambayo mtu
aliyefanikisha jambo la hatari hupewa ili kutukuzwa,baada ya tukio lile maisha
yaliendelea na mke wangu mdogo ndiye aliyebaki nyumbani huku akifurahi sana
kuwa mke pekee aliyebaki nyumbani
Baada mwezi mmoja na nusu kupita tokea tukio la mimi kumuua
mke wangu kule msituni ,siku moja nikiwa natoka kuchunga mifugo yangu jioni ,siku
hiyo nilikuwa na furaha sana hata sikujua ila furaha ilitokana na nini lakini
nilijua lazima kutakuwepo mgeni siku ile maana siku ile nilipokuwa machungani
jicho langu la kulia lilinicheza sana na jisi tulivyokuwa tunaamini ni kuwa
jicho likicheza hasa la kulia lazima kuna mgeni,nikiwa kwenye njia ya kuelekea
nyumbani nikiwa na mifugo yangu kwa mbali kidogo mbele yangu kulikuwepo watu
wawili wanatembea ila waliponiona walisimama na nilipowaona niliogopa
sana,alikuwa mke wangu mkubwa na mama yake
Mume wangu shikamoo,nimerudi na nimekumiss sana na mama
amekuja kututembelea.
Umerudi? Yaani mke….
Vipi mume wangu kwani hutaki nirudi au?
Shikamoo mama..
Marhaba mwanangu za kwako?
Salama tu karibuni sana
Nimeona nije na mwanangu kwa maana tokea siku anarudi
nyumbani alivamiwa akapigwa ila cha kushukuru wasamalia wema walimsaidia
wakamleta hadi nyumbani lakini hadi leo aliyemvamia hatujamjua bado lakini
chakushangaza hakuibiwa chochote alichokuwa nacho na chakushangaza zaidi
alikuwa amefungwa kamba shingoni
Ilinibidi nijifanye kama sijui chochote na nikaonyesha
mshangao mkubwa sana,kutokana na kuwa hatukuwa mbali na nyumbani tulitembea
kidogo na haikuchukua muda tukafika nyumbani ila mke wangu mdogo aliponiona
nimeambatana na mke wangu mkubwa na mama yake aliamua kuingia kwenye nyumba yake
hadi muda wa kulala hakutoka tena nje,mke wangu mkubwa alifika akaanza kufanya
usafi kisha akapika na alipomaliza kupika akatukaribisha wote tule pamoja
chakula cha usiku,lakini mimi na watoto wangu Nkwimba na minza ambao wote
walikuwa ni wadogo hatukwenda kula licha ya kuwa tulikuwa na njaa sana kwa hiyo
siku hiyo ilibidi kulala bila kula kwa maana mtu wa kupika ambaye ni mke mdogo
mama wa watoto wangu wawili hakupika siku hiyo na hatukutaka kabisa kula
chakula cha mke wangu mkubwa tukiwa tunaogopa kuwekewa dawa
Umefuata nini humu?
Nimekuja kulala.
Si uende kwa Malaya wako amekuja na mama yake wachawi hao na
siku ile kumbe hukumuua eti? Kumbe bado unampenda ee?,mi nitaenda kwetu
nikuache ufurahi na kijike chako chembamba kama bamia ya nyongeza.
Usifanye hivyo mke wangu,ukienda utaniacha na nani na mimi
nakupenda.
Nilimbembeleza sana mke wangu usiku ule hadi akakubali kuwa
hataondoka,baada ya miezi kama miwili ilikuwa siku ya jumanne mida ya usiku mke
wangu mdogo alipata uchungu ili ajifungue jambo la kwanza kulifikilia ni
kumpeleka kwenye kituo cha afya lakini yeye alilazimisha nimpeleke kwa mganga
na si hospitali au sehemu yoyote na mimi sikuwa mbishi nikambeba kwenye
baisikeli yangu kwa haraka mpaka kwa mganga,mganga tulimkuta akiwa na watu
wengine akiwa anawahudumia,aliniambia nimpeleke mke wangu kwenye kijumba kidogo
nilipomfikisha tu akanambia nimpishe nikae nje.
Baada ya masaa kama
mawili nilisikia maneno ya mganga ambayo sikuyaelewa ni ya lugha gani,mganga
alikuwa anatamka maneno kwa sauti ya chini kisha anapandisha sauti kama mlevi
vile,lakini baada ya muda kidogo mganga alikuja hadi nilipo kuwa pale nje na mkononi mwake alikuwa ameshikilia mkia wenye
manyonya meusi kama mkia wa nyumbu au mbogo akaniangalia kwa muda kisha
akauloweka ule mkia kwenye maji kisha akaninyunyizia yale maji kwa kutumia ule
mkia maji ambayo sikujua yamechanganywa na nini maana mwili mzima ulianza
kuniwasha na nikaanza kuishiwa nguvu na hatimaye nikaona giza machoni
nikaanguka na kusinzia usingizi mzito sana
Sikujua kuwa nilisinzia kwa muda gani ila nilijikuta kwenye
nyumba ndogo nikiwa nimevuliwa nguo zote isipokuwa tu nguo yangu ya ndani tu na
nilipojipapasa kichwani sikuwa na nywele zilikuwa zimenyolewa zote,nikiwa bado
natafakari pale chini wakaingia watu watatu ambao ni mke wangu,na wanaume
wawili ambao walikuwa wamejifunika nguo nyeusi kuanzia kichwani hadi miguuni na
sikufanikiwa kuziona sura zao na mikononi mwa wale wanaume wawili walikuwa wamebeba
ungo kila mmoja na kwenye kila ungo kulikuwa na kitambaa chekundu kilichokuwa
kinafuka moshi,baada ya muda kama wa dakika tano wale wanaume wawili waliovalia
nguo nyeusi walitoka na kuniacha na mke wangu kwenye kile chumba kidogo.
Wale wanaumme wawili walipotoka nikaanza kumuuliza mke wangu
maswali mengi lakini wakati wote nilipomuuliza maswali aliendelea kuwa kimya tu
hakujibu chochote,nikiwa bado naendelea kumhoji mke wangu,jamaa mmoja kati ya
wale wanaume wawili alirudi na kunisihi nisipige kelele kwani eneo lile kuna
mizimu ilikuwa inafanya kazi na ningeendelea kuongea ingenidhuru nipoteze
fahamu kama ilivyokuwa awali nilipo lala usingizi mzito,muda huo wote nilikuwa
nimevaa nguo ya ndani tu na sikujua ni wapi nguo zangu zingine zilipokuwa
baada ya muda kidogo mganga alikuja akakaa kwenye ngozi ambayo
sikujua ni ya mnyama gani kisha akaniamuru mimi na mke wangu tukae sote
tukafata kila maagizo tuliyopewa,alituamuru tukae tunyoshe miguu tukiwa
tumeangalia upande wa kusini huku tumesogeleana kabisa,baada ya kufanya kila
alichotuagiza mganga akapiga mruzi wale wanaume wawili wenye nguo nyeusi
walikuja na mikononi mwao walikuwa wamembeba mtoto aliyezaliwa walipofika ndani
wakapiga magoti mbele yetu kisha wakafunua nguo walizokuwa wamemfunikia Yule mtoto mchanga nilipomwona
nilifurahi kwa maana alikuwa ni mtoto wa kiume na kwa muda mrefu nilikuwa natamani
nipate mtoto wa kiume lakini muda wote mke wangu hakuonekana kuwa na furaha
yoyote,wale wanaume waliinama kwa muda wa kama dakika mbili kisha wakamweka kwenye
miguu yetu wakaniamuru nimshike kisha wakaondoka tukabaki watatu mimi,mke wangu
na mganga,nilikuwa na shauu sana ya kumshika mwanangu wa kiume,alipowekwa
miguuni mwetu nikapeleka mikono ili nimshike mwanangu kwa shauku kubwa lakini
kilichonishitua mtoto alikuwa wa baridi sana,sauti ya kutisha ya mganga ndiyo
ilinitoa kwenye kumdadisi mwanangu.
umeua!! Umeua !! masanja masanja mbona unakuwa baba mjinga
sijaua mimi! Sijaua kabisa.
Wewe kweli hujaua,nilikuagiza umuue kwa kumnyonga leo
amekuulia mwanao tena wa kiume unaona
raha eti?.
Baada ya maelezo kidogo mganga ilibidi anipe mashariti
mengine ili kuipoza mizimu maana alidai kuwa ilikuwa na hasira sana kutokana na
makosa niliyoyafanya mimi,mganga alipiga mruzi ndani ya muda mfupi wale wanaume
wawili wenye mavazi meusi wakaja wakasimama mbele yetu kisha mganga akaamuru
nisimame na mimi nikasimama kisha mganga akanisihi nikubali kila
watakaloniambia wale wanaume wawili wenye mavazi meusi kisha akawaambia
wanipeleke Mombasa kabla ya jogoo kuwika……………….INAENDELEA
Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159
ReplyDeleteKwa uchawi wa kuungana tena.
Kwa ujanja wa ujauzito.
Kushinda bahati nasibu.
Kushinda kesi mahakamani.
Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.