HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)
HADITHI YA
BABA MASUMBUKO
Mtunzi:PAUL M,YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook:Yahilima PM
SEHEMU YA NNE
Wale wamaume wawili ambao muda wote walikuwa kimya tokea
nifike kwa mganga,waliniamuru niwafuate na mimi nilianza kuwafuata,mmoja alikuwa
mrefu zaidi ya mwenzake na huyu ndiye alikuwa anatuongoza njia kwa maana
alikuwa mbele yetu kisha mimi nikafuatia huku mwingine aliyekuwa mfupi alikuwawa
nyuma yangu kwa hiyo mimi nilikuwa katikati ya wale wanaume wawili,muda wote
tulipokuwa tunatembea hakuna mtu
aliyemwongelesha mwenzake wakati huo mimi nilifuata tu kama ng`ombe asiyejua
anapopelekwa,tulitembea hadi tukavuka mto unaotenganisha kijiji chetu na cha
jirani,baada ya kutembea hatua kama mia hivi tulifika kwenye msitu mdogo wakati
huo wote nilikuwa na mawazo mengi juu ya usafiri upi tutatumia ili kufika Mombasa na huko Mombasa tunafuata nini
usiku huo,gafla mtu aliyekuwa ametutangulia alisimama na sote wawili tuliyemfatia tulisimama,kisha Yule
mtu mrefu aliyekua anatuongoza akamuuliza Yule mfupi
Vipi,unaanza wewe au nianze mimi?
Anza tu mi nitamalizia.
Muda huo sikujua kipi kitafuata baada ya wale watu kuchagua
yupi aanze,nikiwa bado natafakari Yule jamaa mfupi alinikaba shingo na
kuniinamisha kwa nguvu alizidi kuigandamiza mikono yake kwenye kichwa changu kwa
nguvu hadi nikawa sina nguvu kabisa nikabaki nikiwa nimeinama,muda natafakari
juu ya kipi kitafuata yule jamaa mrefu
alikuja nilipokuwa akanivua boksa niliyokuwa nimevaa maana muda wote sikuwa
nimevaa nguo zaidi ya ile boksa tokea nilipovuliwa nguo kwa mganga,nikiwa bado
natafakari nilimwona yule jamaa mrefu akilitupa pembeni lile vazi jeusi na muda
huo nilifanikiwa kuiona sura yake ilikuwa ni sura ambayo sikuwahi kuiona popote
na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuiona sura ile,nilimtazama kwa makini Yule
jamaa kwa harakaharaka alianza kuvua nguo zake hadi akabaki kwenye boksa tu
akaanza kupiga hatua kunisogelea nilipokuwa lakini nilipatwa na wazo kuwa
nataka kutendewa kitendo ambacho mwanaume halisi akitendewa atajutia maishani mwake,Yule
jamaa alipokaribia nilipokuwa nikakusanya nguvu zote nikamsukuma yule jamaa
aliyekuwa amenishikilia kwa haraka sana nikatoka mbio na wale jamaa wakaanza kunifukuza lakini kwa sababu ilikuwa
usiku nilifanikiwa kuwaacha.
Kwa kuwa ilikuwa usiku sikuwaza tena kwenda kwa mganga nilipitiliza hadi nyumbani
kwamgu nilipofika nikaingia chumbani
nikawapita watoto wangu kimyakinya ambao walikuwa wamelala pale sebuleni,taratibu nikaingia chumbani nikavaa
nguo zangu,nikafikilia kipi nifanye nikaona nikiendelea kukaa ndani wale watu
wataweza kunifuatilia hadi nyumbani,nikaamua kutoka ndani ya nyumba nikaenda
nje mbali kidogo na nyumba,baada ya kupita masaa kama mawili kwa mbali nikasikia sauti ya mtu analia
nilipoisikiliza kwa makini niliitambua sauti ile kuwa ni ya mke wangu mdogo na
nilipomchunguza kwa makini mgongoni kwake alikuwa amebeba maiti ya mtoto
aliyejifungua kule kwa mganga wa
kienyeji,ikanibidi nijitokeze kwa lengo
la kushilikiana naye ili tuweze
kuwajulisha watu juu ya tukio la mtoto kuzaliwa akiwa amekufa.
Nilianza kuwapa taarifa majirani hadi inafika saa mbili asubuhi watu wote
walikuwa na taarifa na siku hiyo ikawa ya msiba,muda wa mazishi ulifika,kutokana
na utamaduni wa jamii yetu ilikuwa ni lazima mtoto chini ya miaka akifariki baba yake ni lazima amuwekee kaa la moto
kwenye njia ya haja kubwa mtoto aliyefariki kwa imani ya kutokomeza matukio ya watoto kufariki wakiwa na umri chini ya miaka mitano ili
matatizo kama yale yasijirudie,kama kawaida kaa la moto likaletwa nikapewa mimi
ambaye ni baba wa yule mtoto aliyefariki nikaweka kaa lile kwenye njia ya haja
kubwa ya mtoto baada ya kumaliza utaratibu ule mazishi yakafanyika na kawaida
ya mila na utamaduni pia pale anapofariki mtoto mwenye chini ya miaka mitano
watu huwa hawakai baada ya mazishi ili kuepusha watoto kuendelea kufariki na
kweli baada ya mazishi watu walisambaa.Usiku ulipoingia hali ya kijiji ilikuwa ya ukimya sana ila usiku
ulipofika katikati milio mingi ya fisi
na bundi ilianza kusikia sehemu mbalimbali za kijiji hali ile iliwafanya watu wote
waogope sana usiku ule lakini hali ya utulivu ilirudi pale jogoo wa kwanza
alipowika,watoto wangu wa kike walitoka nje kujisaidia haja ndogo ila walirudi
ndani kwa mbio sana wakanifanya nishituke sana,niliwauliza kuna kipi kimetokea
lakini hakuna hata mmoja aliyenijibu nikaamua kuchungulia dirishani ili nijue
kilichowafanya warudi mbio ndani lakini chakushangaza niliwaona watu wawili
wakiwa kwenye kabuli alimozikwa mwanangu watu wale walikuwa wanafukua kaburi
hali ile iliniogopesha sana,nilikaa kama robo saa ndani nikiwaza kipi nifanye
nikatoka kimya kimya bila wale watu kuniona nikaenda kuwajulisha majirani,baada
ya muda kidogo mimi na majirani tulikuja taratibu hadi karibu na nyumba yangu
tukajificha kwenye miti ya minyaa na muda huo tayari wale wanaume walikuwa
tayari wameshauweka mwili wa mwanangu kwenye mfuko wa sandarusi,wale wanaumme walijaribu
kutumia uchawi ili waweze kuondoka bila mtu kuwaona lakini walishindwa hali
hiyo ilionyesha kuwa walikosea mashariti maana kila mmoja alikuwa anamlaumu
mwenzake kuwa amekiuka masharti,hadi saa moja asubuhi watu wengi walikuwa tayari wamejaa na wale
wanaume waliokuwa wanafukua kabuli kwenye vichwa walikuwa wamevaa vinyago(mask)
ilikuwa ni ngumu kuwatambua ni akina nani, walipouona umati wa watu uliokuwa
umewazunguka walitaka kukimbia lakini walishindwa kutokana na wingi wa watu
waliowazunguka,wanakijiji walipiga yowe na kawaida ya yowe wanaume wote kwenye
kijiji walikukusanyika ndipo uamuzi
ukatolewa na mkuu wa sungusungu kuwa wale watu wapelekwe kwenye mti wa hukumu
ambao ni mti mkubwa kuliko miti yote kwenye kijiji,ilipofika saa nne wazee wa
kijiji na sungusungu wakaja baada ya ukimya kidogo mkuu wa sungusungu akaanza
kungea kwa sauti kubwa na wanakijiji waliokusanyika wakamsikiliza kwa makini
Naomba kila mtu anisikilize,sote hapa ni wanaume hatuogopi
chochote na wanawake wote wako nyumbani,hawa watu tuliowakamata asubuhi hakuna
hata mmoja anayejua ni wapi wanatokea na tunataka watueleze wametokea wapi na
pia vijana wapiganaji mfuateni masalu ambaye ni mke wa kwanza wa masanja pamoja
na mama yake maana hawa ni wachawi na ndiyo wameifanya mvua isinyeshe kwenye
kijij chetu,fanyeni haraka kuwaleta wapuuzi hawa
Sawa mkuu tunawaleta mapema.
Muda ambao mke wangu mkubwa masalu na mama yake wakiwa
wamefatwa wale jamaa waliletwa mbele ya umati wakiwa na mwili wa mwanangu
aliyefariki kwenye mfuko wa sandarusi,kamanda mkuu wa sungusungu akawavua vile
vinyago walivyo vaa kichwani(mask),nilishituka baada ya kuwatambua kuwa ni wale
waliopewa jukumu la kunipeleka Mombasa kisha nikawakimbia,ule mfuko wa
sandarusi ulifunguliwa na watu wote umati walishangaa kuona mtoto mdogo akiwa
amekatwa kichwa na sehemu zake za sili zikiwa zimekatwa pia,lakini wale wanaume
walipoulizwa nani aliyewatuma kuja kufukua maiti ya mtoto yule walishindwa
kutaja jina wakawa kama wamezibwa midomo yao lakini mimi nilijua wazi kuwa ni
mganga ndiye kawatuma.
Nani kawatuma na mnatokea wapi
Aliyetutuma ni……… tumetokea gamboshi
Baada ya muda kidogo wanakijiji wote tulisimama watu
wakashangilia kwa shangwe na mbinja huku sote tukajipanga kwenye msitari na
kila mmoja kama kawaida alikuwa na fimbo yake mkononi,mke wangu wa kwanza na
mama yake waliletwa na kwa mashariti ya kijiji ilibidi tupange mstari mmoja ili
watuhumiwa wapiti kwenye ule mstari kila wanapopita kwenye msitari ni lazima
kila mtu amchape mtuhumiwa fimbo moja moja,mimi kama wanakijiji wenzangu
nilimchapa mke wangu na mama mkwe,na baada ya lile tukio la kuwachapa fimbo
watuhumiwa,watuhumiwa wote wanne walifungwa kwenye mti ili wahukumiwe na uzito
wa hukumu hutokana ukubwa wa kosa,mkuu
wa sungusungu aliuliza kati ya wale wanaumme wawili waliofukua maiti na
wanawake wawili yaani mke wangu na mama mkwe waliotuhumiwa kuifanya mvua
isinyeshe ni wapi wenye kosa kubwa lakini wanakijiji kila mmoja aliangalia
uzito wa kosa kutokana na anavyoona hadi wakaamua kupiga kura ili wapate ni akina
nani wenye kosa,mkuu wa sungusungu alisimama baada ya kura kupigwa
Kutokana na kura
zilizopigwa,huyu mama asiye na mtoto na mama yake ndiyo wenye kosa kubwa maana
wanataka tufe kwa njaa,ila hawa waliofukua mtoto hawana kosa kubwa maana mtu
kama amekufa hana msaada au mnasemaje?
Ndiyooooo, hukumu lazima iwahusu yaani wafe wanajiona
Najua mnaijua hukumu ya hawa watu,ukiwa na kosa kubwa kama hili,
Ndiyoo,wavune walichokipanda
Mbele ya macho yangu nikajionea wale wanaume wawili
wakiachwa huru wakabeba na maiti ya mwanangu wakaondoka huku mkuu wa sungusungu
akidai kuwa eti hawakuwa na kosa na kwa maelezo waliyoyatoa ni kuwa walikuwa
wanatafuta utajiri kupitia ile maiti ya mtoto,baada ya hapo nikaanza kujiuliza
juu ya hukumu ipi ambayo mke wangu mkubwa na mama mkwe watapewa maana hukumu ya
mtu mwenye kosa kubwa kwenye kijiji hukatwa kiungo kimoja kimoja cha mwili wake
kuanzia vidole ya miguu hadi kichwa
mpaka anakufa na viungo vyote huchomwa moto ili apotee kabisa hata mfupa wake
usionekane ili kumfuta kabisa kwenye dunia ya watu hai na mizimu,vijana
waliagizwa wakusanye kuni nao wakafanya hivyo na baada ya kuni kukusanywa yule
mkuu wa sungusungu akaomba akabiziwe upanga wa hukumu na moto ukawashwa kisha akaamuru
watu wote wawe kimya kabisa na hali ya ukimya ikatawala kabisa pale,kwa
kujiamini akaanza kupiga hatua kwenda kwenye sehemu ambayo mke wangu na mama
mkwe walikuwa wamefungwa ………………….INAENDELEA
USACHE KUUFUATILIA MWENDELEZO SEHEMU YA 5
Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159
ReplyDeleteKwa uchawi wa kuungana tena.
Kwa ujanja wa ujauzito.
Kushinda bahati nasibu.
Kushinda kesi mahakamani.
Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.