HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KWANZA (1)

                                                             HADITHI YA

                                                              BABA MASUMBUKO
Mtunzi: PAUL M,YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook yahilima pm
Tembelea http://mla-ukoko.blogspot.com
                                                                 SEHEMU YA KWANZA
Wewe! huyu mwanamke asiyezaa bado hajaleta chakula hadi sasa?,

 nilimuuliza mke wangu mdogo naye akanijibu kuwamke mkubwa hajaleta chakula chochote kisha nikamwagiza mke wangu mdogo afuate chakula maana ilikuwa ni kawaida yangu kula chakula cha wake zangu wote na hata kama nikitoka wiki moja lazima nikute mboga walizokula kwa siku ambazo sikuwepo,baada ya muda mfupi mke wangu mdogo alirudi na nilipomuuliza  kwanini hajaja na chakula hakunijibu chochote moja kwa moja nikajua  atakuwa amejibizana vibaya na mwenzake,nilikura kwa haraka na baada ya kula nilimwita mke wangu mdogo naye akaja karibu na mimi,
nambie mume wangu nikupendaye kwa dhati ila mwenzako mwanamke wako hanipendi yaani leo kanitukana                
mwache tu dawa yake ipo jikoni na lazima atang`oka tu

Halafu mume wangu hii mimba nahisi atakuwa mtoto wa kiume, nataka nikufurahishe sana maana nimekuzalia watoto wawili wa kike sasa unahitaji kidume

Nilitamani nimweleze mke wangu mdogo nilichopanga kumweleza siku ile ila baada ya maelezo yake kuhusu mimba nilishindwa hata kumwambia na siku ile nilipanga kumweleza kuwa nataka kwenda kulala kwa mke mkubwa kwa siku ile kwa maana siku nyingi zilipita bila kulala kwa mke mkubwa,mke mdogo alienda kutandika kitanda akaniacha sebuleni, ghafla nje mbwa walianza kubweka kama kawaida ya maisha ya kijijini ilinibidi nitoke nje kwenda kuangalia kipi mbwa wangu kinawafanya wabweke,ulikuwa ni usiku wenye giza  sana uliotawaliwa na sauti za vyura zilizokuwa zinasikika kutoka kwenye mto unaotenganisha kijiji chetu cha matongo na kijij cha jirani  cha sapiwi mkoani simiyu,kwa mbali maji yalisikika yakipigana vikumbo kwenye mto kutokana na mvua iliyonyesha jioni ya siku ile,nikiwa bado naangalia usalama pale nyumbani nilisogea kwenye zizi la ng`ombe ambao jioni ile ndiyo nilitoka kuwachunga, ghafula mbwa waliokuwa karibu na na mimi walikimbia kuelekea upande wa pili wa zizi  na mimi nikajaribu kuelekea kule  mbwa walipoelekea lakini kabla hata sijasogea zaidi wale mbwa walirudi kwa kasi na kunipita nilipokuwa,sikuwa na lakufanya na kwa sababu sikuwa hata na tochi yakunisaidia kuona kipi kimewafanya mbwa wangu warudi tena kwa kasi hivyo,nilijawa na uoga nikakimbia nikaupalamia mlango dhaifu wa nyumba ya mke wangu mkubwa, nilipofika sebuleni kutokana na utelezi pale sebuleni nikaanguka ,mke wangu alipiga sauti yakuomba msaada kwa maana alijua kavamiwa lakini nilimweleza kuwa ni mimi kwa haraka akaja nilipokuwa nimeanguka.

Mume wangu pole kwa kuanguka jamani, tatizo gani limekupata?

Pumbafu wewe yaani umetega maji ili nianguke si ndiyo
?
Hapana sijakutega mume wangu si leo mvua imenyesha na nyumba imevuja sana.

Sasa ulishindwa kuyatoa? 
                                                                                
Samahani mume wangu nisame……..

Mke wangu hakumalizia maelezo yake nikampiga kofi la usoni kwa haraka akarudi chumbani akaniacha pale sebuleni,aliendelea kulia kwa machungu ila sikujali nikamwamuru awashe taa ya koroboi lakini hakuwasha jambo hilo liliniudhi sana nikajawa na ghadhabu kama mbogo aliyejeruhiwa,nikatoka sebuleni kwa lengo la kwenda kumwongezea kipigo nilipofika chumbani nikapapasa kwenye ndoo ndogo aliyokuwa anatumia kama meza,nikapata kibiriti nikawasha njiti kabla hata sijawasha taa nikamwona mke wangu akitokwa na damu nyingi sana puani na mdomoni jambo hilo lilinitia hofu sana hadi njiti ile ikazimika na nilipowasha njiti ya pili ili niwashe taa aina ya koroboi kwa bahati mbaya haikuwa na mafuta,kutokana na hofu kubwa juu ya damu zinazoendelea kumtoka mke wangu na kilio alichoendelea kukitoa niliamua kuichukua koroboi na kutoka kwenye nyumba ile ili nifuate mafuta kwa mke wangu mdogo,nilitoka nje nikiwa nakimbia bila kujua kumbe alikuwepo mbwa akiwa amejilaza mlangoni nikamparamia nikaanguka na kiatu kimoja cha kata mbuga kikachomoka mguuni lakini sikujali juu ya hilo nikaamka nikakimbia kwa haraka hadi kwenye nyumba ya mke wangu mdogo,

Wewe mwanamke fungua dirisha haraka?

Inakuwaje unagonga hodi dirishani na ulikuwa wapi muda wote huo au ndo ulikuwa na limwanamke lako lisilozaa?

Acha maneno yako nipe mafuta haraka.

Niliamua kuwa mkali ndipo mke wangu mdogo alipoamua kufungua dirisha na kuniwekea mafuta kwenye ile koroboi kisha nikaondoka kwa haraka,nikafika chumbani kwa mke wangu mkubwa nikawasha taa,damu nyingi ilikuwa imemwagika sana mle chumbani,nikatafakari kidogo nikaamua kwenda sebuleni kuchukua maji ya mvua kwenye jagi nikarudi nayo chumbani nikamwagia mke wangu kichwani,damu iliyokuwa inamtoka ikapungua taratibu hadi ikaacha kutoka kabisa kisha nikasafisha mle chumbani kisha nikajitupa kitandani ambapo mke wangu alikuwa tayari amelala.
.
 Mume wangu siku hizi hunipendi,yani tokea umuoe mke mdogo wala hunijali na kumbuka ulimuoa kwa mali tulizotafuta mimi na wewe na badaye umemjengea nyumba nzuri umeezeka mabati kwake umemjengea tena slop kabisa halafu mimi bado niko kwenye nyumba ya nyasi inayovuja kiasi hiki,tazama leo umeteleza na umenipiga mwenzako
.
Nitakujengea na wewe usijali.

Toa uongo wako hapa, kila siku unandanganya tu haya wajengeewenye kuzaa.

 Mke wangu aliongea mengi sana huku akiwa analia hadi nikapitiwa na usingizi kutokana na uchovu wa siku ile,nikiwa bado usingizini nilishituliwa na kitu kizito kilichotua kichani mwangu nilipofungua macho nikakuta mke wangu akiwa ameshikilia rungu

Umenipiga rungu eti? sasa utanijua kuwa mimi ndo masanja halisi

Nimekukomesha na wewe leo maana  umezoea kunipiga tena toka kwangu kalale kwa mkeo unayempenda ambaye huwa anakuzalia watoto tena niache peke yangu na ukinisogelea nitakupa nundu nyingine kama hiyo haijakutosha ili uwe na mapembe kabisa.

Mke wangu mkubwa aliongea kwa hasira nikaamua kutoka chumbani kwake,nikatoka nje kwa hasira jambo la kwanza kulifikilia ni  kwenda kwa mke wangu mdogo lakini nikaona ni vigumu kumshawishi ili aweze kunifungulia usiku ule.Nikajipapasa kichwani nikajikuta nina nundu kubwa iliyotokana na kupigwa kwa rungu na mke wangu mkubwa,hali hii ilinipa uchungu sana na siku zote tokea nikiwa mdogo sikuwahi kukubali kushindwa na mwanamke,nikaamua kurudi kulipiza kisasi nikaingia taratibu mle chumbani kwa bahati nzuri nikamkuta mke wangu akiwa amesinzia nikalitoa rungu karibu yake ambalo hasa ndilo lililokuwa linampa kiburi kisha nikamwamsha na alipoamka tu nikampiga ngumi tumboni,ila kwenye mvurugano mle ndani alibahatisha nafasi akaning`ata mkononi kitendo kile kilioniongezea hasira mara mbili nikamrukia mke wangu  nikamkaba kooni kutokana na kumzidi nguvu hakuwa na uwezo wa kupambana na mimi tena baada ya muda kidogo alipoteza fahamu…………………INAENDELEA

usipitwe na mwendelezo wa hii hadithi like blog kwenye link hiyo chini kisha share  http://mla-ukoko.blogspot.com  
usipitwe                                                     

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)