HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)



                                                                         HADITHI YA
                                                                         BABA MASUMBUKO
Mtunzi: PAUL.M YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook Yahilima PM
                                                                          SEHEMU YA TATU


Japo jambo hilo lilikuwa ni gumu lakini sikuwa na jinsi ya kufanya,kwa haraka nilikiingiza kichwa cha mke wangu mkubwa kwenye ile kamba niliyoiandaa vizuri,lakini nilipotaka  kuivuta kamba ili nimninginize kwenye mti ili ionekane kuwa amejinyonga  nikiwa bado nafikilia kufanya unyama huo,wazo likanijia kichwani kuwa tayari mke wangu atakuwa ameshakufa kutokana na rungu niliyompiga upande wa nyuma ya kichwa,Baada ya tukio hilo nilianza  kutoka kwenye ule msitu kwa tahadhari kubwa huku nikiangalia kama kuna mtu ameniona au la lakini nilibaini kuwa hakuna mtu yoyote aliyeniona,nikatembea hadi nyumbani huku mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka na hofu kubwa moyoni ilinijaa,nilifika nyumbani nikamkuta mke wangu mdogo akiwa mwenye furaha sana na aliponiona tu alinikimbilia.

Mume wangu! Tayari?

Tayari nini?

Umeshammaliza tayari Yule kidudu tayari?

Nilijibu kwa kutikisa kichwa na mke wangu alinipongeza huku akiniita majina ya sifa kama kidume,simba,jabari na mengine mengi ambayo mtu aliyefanikisha jambo la hatari hupewa ili kutukuzwa,baada ya tukio lile maisha yaliendelea na mke wangu mdogo ndiye aliyebaki nyumbani huku akifurahi sana kuwa mke pekee aliyebaki nyumbani

Baada mwezi mmoja na nusu kupita tokea tukio la mimi kumuua mke wangu kule msituni ,siku moja nikiwa natoka kuchunga mifugo yangu jioni ,siku hiyo nilikuwa na furaha sana hata sikujua ila furaha ilitokana na nini lakini nilijua lazima kutakuwepo mgeni siku ile maana siku ile nilipokuwa machungani jicho langu la kulia lilinicheza sana na jisi tulivyokuwa tunaamini ni kuwa jicho likicheza hasa la kulia lazima kuna mgeni,nikiwa kwenye njia ya kuelekea nyumbani nikiwa na mifugo yangu kwa mbali kidogo mbele yangu kulikuwepo watu wawili wanatembea ila waliponiona walisimama na nilipowaona niliogopa sana,alikuwa mke wangu mkubwa na mama yake
Mume wangu shikamoo,nimerudi na nimekumiss sana na mama amekuja kututembelea.

Umerudi? Yaani mke….

Vipi mume wangu kwani hutaki nirudi au?

Shikamoo mama..

Marhaba mwanangu za kwako?

Salama tu karibuni sana 

Nimeona nije na mwanangu kwa maana tokea siku anarudi nyumbani alivamiwa akapigwa ila cha kushukuru wasamalia wema walimsaidia wakamleta hadi nyumbani lakini hadi leo aliyemvamia hatujamjua bado lakini chakushangaza hakuibiwa chochote alichokuwa nacho na chakushangaza zaidi alikuwa amefungwa kamba shingoni

Ilinibidi nijifanye kama sijui chochote na nikaonyesha mshangao mkubwa sana,kutokana na kuwa hatukuwa mbali na nyumbani tulitembea kidogo na haikuchukua muda tukafika nyumbani ila mke wangu mdogo aliponiona nimeambatana na mke wangu mkubwa na mama yake aliamua kuingia kwenye nyumba yake hadi muda wa kulala hakutoka tena nje,mke wangu mkubwa alifika akaanza kufanya usafi kisha akapika na alipomaliza kupika akatukaribisha wote tule pamoja chakula cha usiku,lakini mimi na watoto wangu Nkwimba na minza ambao wote walikuwa ni wadogo hatukwenda kula licha ya kuwa tulikuwa na njaa sana kwa hiyo siku hiyo ilibidi kulala bila kula kwa maana mtu wa kupika ambaye ni mke mdogo mama wa watoto wangu wawili hakupika siku hiyo na hatukutaka kabisa kula chakula cha mke wangu mkubwa tukiwa tunaogopa kuwekewa dawa

Umefuata nini humu?

Nimekuja kulala.

Si uende kwa Malaya wako amekuja na mama yake wachawi hao na siku ile kumbe hukumuua eti? Kumbe bado unampenda ee?,mi nitaenda kwetu nikuache ufurahi na kijike chako chembamba kama bamia ya nyongeza.

Usifanye hivyo mke wangu,ukienda utaniacha na nani na mimi nakupenda.

Nilimbembeleza sana mke wangu usiku ule hadi akakubali kuwa hataondoka,baada ya miezi kama miwili ilikuwa siku ya jumanne mida ya usiku mke wangu mdogo alipata uchungu ili ajifungue jambo la kwanza kulifikilia ni kumpeleka kwenye kituo cha afya lakini yeye alilazimisha nimpeleke kwa mganga na si hospitali au sehemu yoyote na mimi sikuwa mbishi nikambeba kwenye baisikeli yangu kwa haraka mpaka kwa mganga,mganga tulimkuta akiwa na watu wengine akiwa anawahudumia,aliniambia nimpeleke mke wangu kwenye kijumba kidogo nilipomfikisha tu akanambia nimpishe nikae nje.

Baada  ya masaa kama mawili nilisikia maneno ya mganga ambayo sikuyaelewa ni ya lugha gani,mganga alikuwa anatamka maneno kwa sauti ya chini kisha anapandisha sauti kama mlevi vile,lakini baada ya muda kidogo mganga alikuja hadi nilipo kuwa pale nje na  mkononi mwake alikuwa ameshikilia mkia wenye manyonya meusi kama mkia wa nyumbu au mbogo akaniangalia kwa muda kisha akauloweka ule mkia kwenye maji kisha akaninyunyizia yale maji kwa kutumia ule mkia maji ambayo sikujua yamechanganywa na nini maana mwili mzima ulianza kuniwasha na nikaanza kuishiwa nguvu na hatimaye nikaona giza machoni nikaanguka na kusinzia usingizi mzito sana
Sikujua kuwa nilisinzia kwa muda gani ila nilijikuta kwenye nyumba ndogo nikiwa nimevuliwa nguo zote isipokuwa tu nguo yangu ya ndani tu na nilipojipapasa kichwani sikuwa na nywele zilikuwa zimenyolewa zote,nikiwa bado natafakari pale chini wakaingia watu watatu ambao ni mke wangu,na wanaume wawili ambao walikuwa wamejifunika nguo nyeusi kuanzia kichwani hadi miguuni na sikufanikiwa kuziona sura zao na mikononi mwa wale wanaume wawili walikuwa wamebeba ungo kila mmoja na kwenye kila ungo kulikuwa na kitambaa chekundu kilichokuwa kinafuka moshi,baada ya muda kama wa dakika tano wale wanaume wawili waliovalia nguo nyeusi walitoka na kuniacha na mke wangu kwenye kile chumba kidogo.
Wale wanaumme wawili walipotoka nikaanza kumuuliza mke wangu maswali mengi lakini wakati wote nilipomuuliza maswali aliendelea kuwa kimya tu hakujibu chochote,nikiwa bado naendelea kumhoji mke wangu,jamaa mmoja kati ya wale wanaume wawili alirudi na kunisihi nisipige kelele kwani eneo lile kuna mizimu ilikuwa inafanya kazi na ningeendelea kuongea ingenidhuru nipoteze fahamu kama ilivyokuwa awali nilipo lala usingizi mzito,muda huo wote nilikuwa nimevaa nguo ya ndani tu na sikujua ni wapi nguo zangu zingine zilipokuwa
baada ya muda kidogo mganga alikuja akakaa kwenye ngozi ambayo sikujua ni ya mnyama gani kisha akaniamuru mimi na mke wangu tukae sote tukafata kila maagizo tuliyopewa,alituamuru tukae tunyoshe miguu tukiwa tumeangalia upande wa kusini huku tumesogeleana kabisa,baada ya kufanya kila alichotuagiza mganga akapiga mruzi wale wanaume wawili wenye nguo nyeusi walikuja na mikononi mwao walikuwa wamembeba mtoto aliyezaliwa walipofika ndani wakapiga magoti mbele yetu kisha wakafunua nguo walizokuwa wamemfunikia Yule mtoto mchanga nilipomwona nilifurahi kwa maana alikuwa ni mtoto wa kiume na kwa muda mrefu nilikuwa natamani nipate mtoto wa kiume lakini muda wote mke wangu hakuonekana kuwa na furaha yoyote,wale wanaume waliinama kwa muda wa kama dakika mbili kisha wakamweka kwenye miguu yetu wakaniamuru nimshike kisha wakaondoka tukabaki watatu mimi,mke wangu na mganga,nilikuwa na shauu sana ya kumshika mwanangu wa kiume,alipowekwa miguuni mwetu nikapeleka mikono ili nimshike mwanangu kwa shauku kubwa lakini kilichonishitua mtoto alikuwa wa baridi sana,sauti ya kutisha ya mganga ndiyo ilinitoa kwenye kumdadisi mwanangu.

umeua!! Umeua !! masanja masanja mbona unakuwa baba mjinga

sijaua mimi! Sijaua kabisa.

Wewe kweli hujaua,nilikuagiza umuue kwa kumnyonga leo amekuulia  mwanao tena wa kiume unaona raha eti?.

Baada ya maelezo kidogo mganga ilibidi anipe mashariti mengine ili kuipoza mizimu maana alidai kuwa ilikuwa na hasira sana kutokana na makosa niliyoyafanya mimi,mganga alipiga mruzi ndani ya muda mfupi wale wanaume wawili wenye mavazi meusi wakaja wakasimama mbele yetu kisha mganga akaamuru nisimame na mimi nikasimama kisha mganga akanisihi nikubali kila watakaloniambia wale wanaume wawili wenye mavazi meusi kisha akawaambia wanipeleke Mombasa kabla ya jogoo kuwika……………….INAENDELEA
                                                                               

Comments

  1. Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159

    Kwa uchawi wa kuungana tena.
    Kwa ujanja wa ujauzito.
    Kushinda bahati nasibu.
    Kushinda kesi mahakamani.
    Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
    VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KWANZA (1)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)