HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)



                                                                                       HADITHI YA
                                                                                     BABA MASUMBUKO

Mtunzi:PAUL M,YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook:Yahilima PM
                                                                                     SEHEMU YA NNE
Wale wamaume wawili ambao muda wote walikuwa kimya tokea nifike kwa mganga,waliniamuru niwafuate na mimi nilianza kuwafuata,mmoja alikuwa mrefu zaidi ya mwenzake na huyu ndiye alikuwa anatuongoza njia kwa maana alikuwa mbele yetu kisha mimi nikafuatia huku mwingine aliyekuwa mfupi alikuwawa nyuma yangu kwa hiyo mimi nilikuwa katikati ya wale wanaume wawili,muda wote tulipokuwa tunatembea  hakuna mtu aliyemwongelesha mwenzake wakati huo mimi nilifuata tu kama ng`ombe asiyejua anapopelekwa,tulitembea hadi tukavuka mto unaotenganisha kijiji chetu na cha jirani,baada ya kutembea hatua kama mia hivi tulifika kwenye msitu mdogo wakati huo wote nilikuwa na mawazo mengi juu ya usafiri upi tutatumia ili  kufika Mombasa na huko Mombasa tunafuata nini usiku huo,gafla mtu aliyekuwa ametutangulia alisimama na  sote wawili tuliyemfatia tulisimama,kisha Yule mtu mrefu aliyekua anatuongoza akamuuliza Yule mfupi

Vipi,unaanza wewe au nianze mimi?

Anza tu mi nitamalizia.

Muda huo sikujua kipi kitafuata baada ya wale watu kuchagua yupi aanze,nikiwa bado natafakari Yule jamaa mfupi alinikaba shingo na kuniinamisha kwa nguvu alizidi kuigandamiza mikono yake kwenye kichwa changu kwa nguvu hadi nikawa sina nguvu kabisa nikabaki nikiwa nimeinama,muda natafakari juu ya kipi kitafuata  yule jamaa mrefu alikuja nilipokuwa akanivua boksa niliyokuwa nimevaa maana muda wote sikuwa nimevaa nguo zaidi ya ile boksa tokea nilipovuliwa nguo kwa mganga,nikiwa bado natafakari nilimwona yule jamaa mrefu akilitupa pembeni lile vazi jeusi na muda huo nilifanikiwa kuiona sura yake ilikuwa ni sura ambayo sikuwahi kuiona popote na ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuiona sura ile,nilimtazama kwa makini Yule jamaa kwa harakaharaka alianza kuvua nguo zake hadi akabaki kwenye boksa tu akaanza kupiga hatua kunisogelea nilipokuwa lakini nilipatwa na wazo kuwa nataka kutendewa kitendo ambacho mwanaume halisi akitendewa atajutia maishani mwake,Yule jamaa alipokaribia nilipokuwa nikakusanya nguvu zote nikamsukuma yule jamaa aliyekuwa amenishikilia kwa haraka sana nikatoka mbio na  wale jamaa  wakaanza kunifukuza lakini kwa sababu ilikuwa usiku nilifanikiwa kuwaacha.
Kwa kuwa ilikuwa usiku sikuwaza tena  kwenda kwa mganga nilipitiliza hadi nyumbani kwamgu nilipofika  nikaingia chumbani nikawapita watoto wangu kimyakinya ambao walikuwa wamelala pale  sebuleni,taratibu nikaingia chumbani nikavaa nguo zangu,nikafikilia kipi nifanye nikaona nikiendelea kukaa ndani wale watu wataweza kunifuatilia hadi nyumbani,nikaamua kutoka ndani ya nyumba nikaenda nje mbali kidogo na nyumba,baada ya kupita masaa kama  mawili kwa mbali nikasikia sauti ya mtu analia nilipoisikiliza kwa makini niliitambua sauti ile kuwa ni ya mke wangu mdogo na nilipomchunguza kwa makini mgongoni kwake alikuwa amebeba maiti ya mtoto aliyejifungua  kule kwa mganga wa kienyeji,ikanibidi nijitokeze  kwa lengo la  kushilikiana naye ili tuweze kuwajulisha watu juu ya tukio la mtoto kuzaliwa akiwa amekufa.
Nilianza kuwapa taarifa majirani  hadi inafika saa mbili asubuhi watu wote walikuwa na taarifa na siku hiyo ikawa ya msiba,muda wa mazishi ulifika,kutokana na utamaduni wa jamii yetu ilikuwa ni lazima mtoto chini ya miaka akifariki  baba yake ni lazima amuwekee kaa la moto kwenye njia ya haja kubwa mtoto aliyefariki kwa imani ya kutokomeza  matukio ya watoto kufariki  wakiwa na umri chini ya miaka mitano ili matatizo kama yale yasijirudie,kama kawaida kaa la moto likaletwa nikapewa mimi ambaye ni baba wa yule mtoto aliyefariki nikaweka kaa lile kwenye njia ya haja kubwa ya mtoto baada ya kumaliza utaratibu ule mazishi yakafanyika na kawaida ya mila na utamaduni pia pale anapofariki mtoto mwenye chini ya miaka mitano watu huwa hawakai baada ya mazishi ili kuepusha watoto kuendelea kufariki na kweli baada ya mazishi watu walisambaa.Usiku ulipoingia hali ya  kijiji ilikuwa ya ukimya sana ila usiku ulipofika katikati milio mingi ya  fisi na bundi ilianza kusikia sehemu mbalimbali za kijiji hali ile iliwafanya watu wote waogope sana usiku ule lakini hali ya utulivu ilirudi pale jogoo wa kwanza alipowika,watoto wangu wa kike walitoka nje kujisaidia haja ndogo ila walirudi ndani kwa mbio sana wakanifanya nishituke sana,niliwauliza kuna kipi kimetokea lakini hakuna hata mmoja aliyenijibu nikaamua kuchungulia dirishani ili nijue kilichowafanya warudi mbio ndani lakini chakushangaza niliwaona watu wawili wakiwa kwenye kabuli alimozikwa mwanangu watu wale walikuwa wanafukua kaburi hali ile iliniogopesha sana,nilikaa kama robo saa ndani nikiwaza kipi nifanye nikatoka kimya kimya bila wale watu kuniona nikaenda kuwajulisha majirani,baada ya muda kidogo mimi na majirani tulikuja taratibu hadi karibu na nyumba yangu tukajificha kwenye miti ya minyaa na muda huo tayari wale wanaume walikuwa tayari wameshauweka mwili wa mwanangu kwenye mfuko wa sandarusi,wale wanaumme walijaribu kutumia uchawi ili waweze kuondoka bila mtu kuwaona lakini walishindwa hali hiyo ilionyesha kuwa walikosea mashariti maana kila mmoja alikuwa anamlaumu mwenzake kuwa amekiuka masharti,hadi saa moja asubuhi  watu wengi walikuwa tayari wamejaa na wale wanaume waliokuwa wanafukua kabuli kwenye vichwa walikuwa wamevaa vinyago(mask) ilikuwa ni ngumu kuwatambua ni akina nani, walipouona umati wa watu uliokuwa umewazunguka walitaka kukimbia lakini walishindwa kutokana na wingi wa watu waliowazunguka,wanakijiji walipiga yowe na kawaida ya yowe wanaume wote kwenye kijiji walikukusanyika  ndipo uamuzi ukatolewa na mkuu wa sungusungu kuwa wale watu wapelekwe kwenye mti wa hukumu ambao ni mti mkubwa kuliko miti yote kwenye kijiji,ilipofika saa nne wazee wa kijiji na sungusungu wakaja baada ya ukimya kidogo mkuu wa sungusungu akaanza kungea kwa sauti kubwa na wanakijiji waliokusanyika wakamsikiliza kwa makini

Naomba kila mtu anisikilize,sote hapa ni wanaume hatuogopi chochote na wanawake wote wako nyumbani,hawa watu tuliowakamata asubuhi hakuna hata mmoja anayejua ni wapi wanatokea na tunataka watueleze wametokea wapi na pia vijana wapiganaji mfuateni masalu ambaye ni mke wa kwanza wa masanja pamoja na mama yake maana hawa ni wachawi na ndiyo wameifanya mvua isinyeshe kwenye kijij chetu,fanyeni haraka kuwaleta wapuuzi hawa

Sawa mkuu tunawaleta mapema.

Muda ambao mke wangu mkubwa masalu na mama yake wakiwa wamefatwa wale jamaa waliletwa mbele ya umati wakiwa na mwili wa mwanangu aliyefariki kwenye mfuko wa sandarusi,kamanda mkuu wa sungusungu akawavua vile vinyago walivyo vaa kichwani(mask),nilishituka baada ya kuwatambua kuwa ni wale waliopewa jukumu la kunipeleka Mombasa kisha nikawakimbia,ule mfuko wa sandarusi ulifunguliwa na watu wote umati walishangaa kuona mtoto mdogo akiwa amekatwa kichwa na sehemu zake za sili zikiwa zimekatwa pia,lakini wale wanaume walipoulizwa nani aliyewatuma kuja kufukua maiti ya mtoto yule walishindwa kutaja jina wakawa kama wamezibwa midomo yao lakini mimi nilijua wazi kuwa ni mganga ndiye kawatuma.

Nani kawatuma na mnatokea wapi

Aliyetutuma ni……… tumetokea gamboshi

Baada ya muda kidogo wanakijiji wote tulisimama watu wakashangilia kwa shangwe na mbinja huku sote tukajipanga kwenye msitari na kila mmoja kama kawaida alikuwa na fimbo yake mkononi,mke wangu wa kwanza na mama yake waliletwa na kwa mashariti ya kijiji ilibidi tupange mstari mmoja ili watuhumiwa wapiti kwenye ule mstari kila wanapopita kwenye msitari ni lazima kila mtu amchape mtuhumiwa fimbo moja moja,mimi kama wanakijiji wenzangu nilimchapa mke wangu na mama mkwe,na baada ya lile tukio la kuwachapa fimbo watuhumiwa,watuhumiwa wote wanne walifungwa kwenye mti ili wahukumiwe na uzito wa hukumu hutokana  ukubwa wa kosa,mkuu wa sungusungu aliuliza kati ya wale wanaumme wawili waliofukua maiti na wanawake wawili yaani mke wangu na mama mkwe waliotuhumiwa kuifanya mvua isinyeshe ni wapi wenye kosa kubwa lakini wanakijiji kila mmoja aliangalia uzito wa kosa kutokana na anavyoona hadi wakaamua kupiga kura ili wapate ni akina nani wenye kosa,mkuu wa sungusungu alisimama baada ya kura kupigwa

Kutokana na  kura zilizopigwa,huyu mama asiye na mtoto na mama yake ndiyo wenye kosa kubwa maana wanataka tufe kwa njaa,ila hawa waliofukua mtoto hawana kosa kubwa maana mtu kama amekufa hana msaada au mnasemaje?

Ndiyooooo, hukumu lazima iwahusu yaani wafe wanajiona

Najua mnaijua hukumu ya hawa watu,ukiwa na kosa kubwa kama hili,

Ndiyoo,wavune walichokipanda

Mbele ya macho yangu nikajionea wale wanaume wawili wakiachwa huru wakabeba na maiti ya mwanangu wakaondoka huku mkuu wa sungusungu akidai kuwa eti hawakuwa na kosa na kwa maelezo waliyoyatoa ni kuwa walikuwa wanatafuta utajiri kupitia ile maiti ya mtoto,baada ya hapo nikaanza kujiuliza juu ya hukumu ipi ambayo mke wangu mkubwa na mama mkwe watapewa maana hukumu ya mtu mwenye kosa kubwa kwenye kijiji hukatwa kiungo kimoja kimoja cha mwili wake  kuanzia vidole ya miguu hadi kichwa mpaka anakufa na viungo vyote huchomwa moto ili apotee kabisa hata mfupa wake usionekane ili kumfuta kabisa kwenye dunia ya watu hai na mizimu,vijana waliagizwa wakusanye kuni nao wakafanya hivyo na baada ya kuni kukusanywa yule mkuu wa sungusungu akaomba akabiziwe  upanga wa hukumu na moto ukawashwa kisha akaamuru watu wote wawe kimya kabisa na hali ya ukimya ikatawala kabisa pale,kwa kujiamini akaanza kupiga hatua kwenda kwenye sehemu ambayo mke wangu na mama mkwe walikuwa wamefungwa ………………….INAENDELEA
                                                                               
USACHE KUUFUATILIA MWENDELEZO SEHEMU YA 5

Comments

  1. Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159

    Kwa uchawi wa kuungana tena.
    Kwa ujanja wa ujauzito.
    Kushinda bahati nasibu.
    Kushinda kesi mahakamani.
    Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
    VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KWANZA (1)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)