HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KUMI NA MOJA(11)
HADITHI YA
BABA
MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook:Yahilima PM
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Nilipoanza kunyata ili
nikatekeleze unyama nikaona si sawa nikimuua kwa njia rahisi maana niliogopa
majirani kama watasikia kelele,wazo lililonijia ambalo lilikuwa sahihi ni
kwenda kwenye nyumba ya jirani maana pale kulikuwepo na nyumba iliyoezekwa
nyasi ambayo huwa wanaitumia kama jiko na kulazia mifugo yao uamzi niliokuwa
nao ni kwenda kuichoma ile nyumba ili hata kama nikiwa natekeleza mauaji kelele
za kilio kisisikike,nilienda hadi kwa jirani kutokana na ile nyumba kuwa karibu
na shamba,nilienda taratibu nikawasha njiti tatu za kibiriti kwa mkupuo
nikazirusha juu ya ile nyumba bila
kuchelewa nikakimbia kwa kasi kuja kummaliza mke wangu kadri nilivyozidi
kuisogelea nyumba ya mke wangu mkubwa kelele za kuomba msaada zilisikika kwenye
nyumba niliyoichoma moto na ndani ya muda mfupi uliopita,kila upande wa kijiji
yowe zilisikika kama kawaida wanakijiji walizidi kusogea ili kutoa msaada
kwenye ile nyumba ya jirani niliyoichoma,
Nilipoona kuwa wananchi wameweka
umakini kwenye tukio la kuungua kwa nyumba kwa upande wangu niliona kuwa ile
ilikuwa ni nafasi ya mimi kutekeleza
unyama nilioupanga,nikaanza
kutembea kwa kunyata hadi mlangoni kwenye nyumba ya mke wangu mkubwa,kwa
msaada wa mwanga wa taa ya koroboi nilimwona mke wangu akiwa sebuleni muda huo
alikuwa anaendelea kula taratibu,nilijawa na hasira sana hasa nilipokumbuka
mambo aliyonitendea,nilirudi nyuma kama hatua tatu hivi usawa wa
mlango,nikavuta kasi nikahesabu mara tatu nikauparamia ule mlango na kwa bahati
nzuri komeo ilikatika na mlango ukafunguka na kabla mke wangu hajasimama
niliingia kwa kasi na bila hata kufikilia niliinua panga nililokuwa
nalo nikalishusha kwa nguvu kwa bahati nzuri lilitua katikati ya kichwa chake na kukitenganisha kama vile
chungwa linapokatwa nikamkagua kama alikuwa amefariki tayari nikajilizisha kuwa
tayari alikuwa amesha kufa,nikatoka taratbu kwenye ile nyumba kwa bahati nzuri
hakuna mtu aliyekuwa ananiona.
Baada ya mauaji yale nikatokomea kuelekea kwenye mto wa karibu ili
nikaoge na nikajisafishe,nilifika mtoni nikaoga na nikalisafisha
nilipohakikisha kuwa usafi umekamilika
nikavaa nguo zangu vizuri na kuanza safari ya kuelekea sehemu ambayo mganga
aliniambia tukutane baada ya kukamilisha lile zoezi nilitembea kwa haraka na
baada ya muda mfupi nilifika sehemu husika.
Sasa masanja umekuwa
masanja yaani umekuwa mweupe kabisa itabidi uniletee ng`ombe watatu ili uwe
kamili kabisa
Sasa mganga nilete
ng`ombe wa nini we nipe dawa kama tulivyoelewana,mbona unabadilisha maelezo
Najua hujui na
mashariti ya uganga huyajui vizuri unakichwa kigumu
Muda ule naendelea
kuongea na Yule mganga kadiri muda ulivyozidi kusogea mbele chuki juu ya Yule
mganga ilizidi hadi nikashindwa kujizuia hadi machozi yakawa yananitoka
mfululizo sikujua kwa nini,muda huo mimi nilikuwa nimesimama wima na mwili
ulikuwa umekakamaa sana na jasho lilizidi kunitoka sana,mganga alikuwa amekaa
ila macho yake yalikuwa yakinitazama na nilivyomtazama kwa makini nikamwona
akiwa na hofu sana sikujua kwanini anahofu hivyo na pale nilipomtazama sana
hasira zilinijaa nikarusha ngumi kutoka kwenye mkono wangu wa kulia kutokana na
uzito wa ngumi ile mganga alianguka chini,bila hata kuuliza chochote mganga akaanza kujitetea na hapo ndipo nikaona
ni njia nzuri ya kumdadisi,nikachomoa lile panga nililolitumia kumuulia mke
wangu,nikakumbuka mambo yote mabaya aliyonitendea Yule mganga ikiwemo kutaka
kuniua kule mlimani akiwa na watu wake,nikakumbuka mtego alionifanyia hadi
nikaenda gamboshi,sikutaka kwendelea kufikilia nikalishusha panga kwa nguvu
alipokuwa ameinama pale chini kwa bahati nzuri alifanikiwa kulikwepa na
nilipomwangalia usoni roho ya huruma iliniingia,nikamshika kwa nguvu
nikamkalisha kwenye jiwe lililokuwa kando,mganga aliniangalia kwa muda kidogo
ila hasira nilizokuwa nazo mwanzoni zikanijia tena,nikampiga kofi zito la usoni
kisha mganga akaanza kueleza jambo jipya kabisa ambalo lilinichanganya zaidi na
hilo ndiyo linalofanya nikusimulie kisa hiki
Sema haraka,nitakukata
mapingili pingili
Mke wako mdogo
Mke wangu mdogo kafanya
nini?
Mke wako mdogo kabla
hujamuoa alikuja nyumbani kwangu akiwa na shida,na shida yenyewe alikuwa
anatafuta dawa ili apate mwanaume wa kumuoa,nilimpa masharti kabla ya kumpa
dawa ilibidi atafute mtu aliyeolewa ambayo bado hajazaa kisha achote mchanga
kwenye nyayo za miguu za huyo mtu,alilifanikisha zoezi hilo kwa muda mfupi na
kwa bahati mbaya alichotza mchanga kwenye nyayo alimopita mke wako mkubwa
masalu,alileta ule mchanga nikauwekea dawa ambayo ilikufanya wewe uanze
kumchukia mkeo mkubwa tofauti na hilo pia tulimfunga mkeo mkubwa uzazi ili
asiweze kuzaa na kweli alishindwa kupata ujauzito hali ambayo wewe
ilikuchanganya akili hadi ukaamua kutafuta mke mwingine na kwa kuwa lengo langu
na mkeo mdogo kabla ya kumuoa lilikuwa kutafuta mwanaume atakayemuoa mkeo
mdogo,tulikufanyia dawa kisha wewe ukawa huoni
wanawake wengine zaidi ya mkeo mdogo ambaye kweli baada ya muda
ulimuaoa, jambo ambalo ulikuwa unalitaka ambao ni kupata watoto ulifanikiwa
kupata watoto wa kike,kutokana na mashariti ya dawa na mizimu mkeo mdogo
hakutakiwa kuzaa mtoto wa kiume na ndiyo maana watoto wote kutoka kwa mkeo
mdogo ni wakike wote na ukikumbuka siku ambayo mkeo mdogo alizaa mtoto wa kiume
mbele yangu,mimi na huyo mkeo tuimuua Yule mtoto kisha wewe tulikulewesha kwa
dawa na hukujua lolote lililoendela hadi tulipomaliza mipango yetu na wewe
ulipata fahamu ulikuta mwanao tayari ameshakufa.naomba ujue kuwa hata wale
watoto wa kike siyo wako ila wale watoto ni wangu mimi mganga na mkeo mdogo
tulikuwa tunakutana mara kwa mara na kushiliki tendo la ndoa ila wewe hukujua
hilo pia ulikosea kuuza ng`ombe zile tatu ili umpeleke shule masumbuko jambo
hili ndiyo liliibua hasira tukaanza kuishambulia familia yako tena kwa sababu
ile mali siyo yako bali ni yangu na mkeo mdogo, na tulikufanyia dawa mbegu zako
za kiume zikawa hazina nguvu kabisa hili lilifanywa na mkeo mdogo uliyemwamini
sana,alikunyoa nywele zako za sehemu za sili na akachukua mbegu zako akaleta
tukachanganya kwenye dawa.uwezo wa Mungu ni mkubwa alikusaidia wewe na mkeo
mkubwa mkampata mtoto mliyemuita Masumbuko,kitendo cha nyinyi kupata mtoto wa
kiume kilitukera sana na tukaifanya umchukie mkeo mkubwa zaidi ya awali maana
tulitumia kivuli cha sura yake ili aonekane mchawi,wewe kwa macho yako ya
kawaida ulimuona mkeo kwenye sehemu mbalimbali na alionyesha dalili zote za
uchawi lakini yule hakuwa yeye bali ni mimi na mkeo mdogo tulijificha kwenye
kivui cha sura yake ili umchukie hadi umemuua leo kwa mkono wako ila kusema
ukweli mkeo mkubwa uliyemuua hajui dawa wala haujui uchawi ila mkeo mdogo ndiye
mchawi,na tambua kuwa mwanao masumbuko tumemtoa kafara gamboshi ili tupate madaraka
Baada ya maelezo hayo
marefu yaliyouchoma moyo wangu kwenye kila neno,mganga aliomba nimsamehe akiwa
bado anaendelea kunisihi nimsamehe,niliinyosha mikono yangu alipokuwa amekaa
nayeye akaileta kwangu ila kabla haijanifikia nilichomoa panga nikalivulumisha
kwa nguvu vidole vyote kumi vya mikono niliviona chini pale,muda huo sikuwa na
huruma niliushika ule upanga kwa mikono miwili na kwa nguvu zangu zote
nilimkata Yule mganga kwenye mapingiili matatu kisha lile panga nikalisimika
pembeni ya mwili wa mganga na hiyo ndiyo sababu ya mimi kukimbilia Dar hadi leo
naokota makopo sina mbele wala nyuma popote utakaponiona usiniite Masanja
kifulambute ila niiteBaba Masumbuko na cha zaidi nakusihi usiamini waganga wa
kienyeji wengi ni waongo muamini MUNGU tu.
*******************MWISHO*********************
PAUL M,YAHILIMA
0788624797
0765084515
yahilimap@gmail.com
Comments
Post a Comment