HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TISA (9)
HADITHI YA
BABA MASUMBUKO
Mwaandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook:Yahilima PM
SEHEMU YA TISA
Baada ya kusikia ile amri ikiamuru
nikamatwe na nikiwa msumbufu niuliwe niliogopa sana ila sikukata tama na
dhamira yangu ya kutoroka ilikuwa palepale nikaanza kuteremka kutoka juu ya
mlima kwa kasi sana lakini nilipobakiza eneo dogo tu ili nifike chini kabisa ya
ule mlima na matumaini ya kutorka yakiwa yamenijaa nikasimama kwa sekunde
kadhaa nyuma kama kuna anayenifuatilia lakini nikabaini kuwa hakukuwepo mtu
anayenifukuza lakini nilipotazama mbele nilipokuwa naenda ambako ndiyo chini
kabisa ya mlima nikaona kundi la watu likiwa linakuja kwa kasi na baadhi walikuwa wameanza kupanda
ule mlima huku wamewasha mwenge na kwa wakati huu wale watu wenye mwenge
walikuwa wengi zaidi na walikuwa wanaimba lakini walipofika kwenye mlima wakawa kimya na ule moto waliokuwa nao
wakauzima kisha giza totoro liliufunika mlima wote,jambo la kushukuru mkononi
nilikuwa na tochi lakini sikuweza hata kuiwasha nikaamua kurudi kwa haraka juu kabla sijafika eneo la
juu kabisa kwenye kilele cha ule mlima ambapo ndipo mganga nilimwacha nikazunguka
kwa haraka nyuma ya mlima ambako kulikuwepo shimo ambalo nilikuwa nimeshaliona
siku za nyuma nikatembea kwa makini ili sauti ya nyayo zangu asisikie mtu na
kwa bahati nzuri nikafanikiwa kufika kwenye lile pango sikujali kama wameniona
au la nikaingia kwenye lile shimo na sikujali nitakutana na hatari gani kwenye
lile shimo refu bila kupoteza muda nikazama kwenye lile shimo nikawasha tochi
nikaangalia kwenye kila sehemu kama kuna hatari yoyote lakini sikuona hatari
zaidi ya popo wengi tu,nikiwa bado natafakari niliona mwanga kwa nje na mlima
wote ukawa unaonekana hali hiyo ilinifanya nijue kuwa wale watu wameshapanda kwenye mlima na
wameshauzunguka wote,hata baada ya mwanga kuonekana kwenye ule mlima hakuna mtu
aliyeweza kusikika akiwa anaongea chochote,ila baada ya dakika chache nje ya
shimo nililojificha niliona kivuli cha mtu anapita lakini sikujua ni nani
nilijawa na hofu kubwa nikajua nilipokuwa ninaingia kwenye shimo labda walikuwa
wameniona na kutokana na hofu mkojo ukanitoka bila hata ya kujua na mwili wote
ulikuwa umelowana kwa jasho,muda huo niliona kabisa siku yangu ya kufa itakuwa
imefika japo tokea nizaliwe sijawahi kuingia kanisani hata tu kukanyaga mlangoni
wala msikiti sikuwahi kuingia lakini nilimuomba sana Mungu aniepushe na watu
wale wabaya.
Mimi ndo mganga ganungo ga walwa
ishiishi lya boshishi mabogota gaza.
Ndiyo mkuu!
Nilipowaambia mkamateni mlifanya
uzembe sasa yuko wapi? Narudia fanyeni juu chini mumkamate
Ndiyo mkuu!
Aje mzima au amekufa sawa?
Sawa mkuu!
Sauti iliyosikika nilikuwa naijua
vyema,alikuwa ni mganga wa kienyeji na baada tu ya kutoa ile amri watu waliokuwa
kwenye eneo lile wakasikia wanatawanyika na ila sauti ya mganga ikaendelea
kusikika pale pale na nikasikia anaomba mizimu yake ili imuonyeshe
nilipo,nikiwa bado nayasikiliza maneno ya mganga wazo likanijia kwa haraka wazo
la kuingia zaidi kwenye lile shimo moja
kwa moja safari nisiyoijua mwisho wake huku nikimwomba Mungu kila hatua
ninayopiga ili iwe ya kheri kusitokee mnyama au mdudu wa kunidhuru,kulikuwepo na shimo refu na
upana wake ulitosha kabisa kupita ila kwa mwendo wa kuinama,muda wote tochi
niliyokuwa nayo nikamulika mbele nilipokuwa naelekea na kwenye mkono wa kushoto
nikabeba mawe ya tahadhari ili chochote kitakachojitokeza niweze kupambana
nacho na kadiri muda ulivyozidi kwenda hofu ilizidi kunijaa nikaanza kusali dua
yangu ya mwisho na nikamuomba sana Mungu anisamehe makosa yangu yote,baada ya
mwendo kama wa saa moja nikachoka sana kutokana na mwendo wa kuinama ikanibidi
niangalie sehemu yenye usalama wa kutosha ili nipumzike baada ya kuhakikisha
kuwa eneo lile ni salama nikakaa kwenye jiwe moja nikakaa,muda wote sikutaka
kabisa niruhuusu usingizi unipitie lakini cha ajabu usingizi ukanipitia
nikasinzia kilichonishitua ni maumivu makali niliyoyapata kwenye kidole kikubwa
cha mguu wa kulia,maumivu yale yakanifanya nifumbue macho kwa haraka nikamwona
ng`e akiwa anatokomea kwenye jiwe la jirani na nilipoweka mguu moja kwa moja
nikajua aliyenigata ni ng`e na haikuwa mara ya kwanza kung`atwa na
ng`e,nikalifunua lile jiwe alimokimbilia Yule ng`e kwa bahati nzuri nikamkuta
nikachukua jiwe dogo nikampiga hadi akafa kisha nikaukata mkia wake ambao ndiyo
huwa anatumia kung`atia na ndiyo wenye sumu kisha nikautafuna nikameza kidogo
na mabaki yake nikabandika kwenye sehemu niliyong`atwa,baada ya muda kama nusu
saa maumivu yakaisha,sikutaka kupoteza muda nikaanza safari tena sikuchukua
muda sana nikiwa kwenye lile shimo kwa mbali nikaona mwanga nikazidi kupata
hofu sana juu ya nini kipo kwenye ule mwanga kwani nikajua wale watu
wamezunguka wananisubiria upande wa pili wa lilie shimo,sikutaka kurudi nyuma
nikasogea mbele tu lakini jambo la kushukuru kumbe ule mwanga niliouona ulikuwa
ni mwanga wa jua,nikasogea mpaka kwenya mlango lile shimo nikaangalia pande
zote lakini sikuona mtu wala kitu cha hatari,nikatoka kwenye lile shimo mida ya
saa moja asubuhi.
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
Baada ya maisha yenye
visa kama vile niliacha kusikiliza mambo ya waganga nikaamua kuitunza familia
yangu nikiwa pamoja na wake zangu wote hadi watoto wangu wale wawili wa kike
wakabahatika kuolewa na nikapata kiasi kikubwa cha ng`ombe jambo ambalo
lilinifurahisha sana,mwanangu wa kiume masumbuko muda wale dada zake wanaolewa
yeye ndiyo kwanza matokeo ya kuhitimu darasa la saba yalikuwa yametoka na
alichaguliwa kwenda kwenye shule ya sekondari ya kata inayoitwa sapiwi
secondary mkoani simiyu,muda ulipofika wa kwenda shule niauza ng`ombe watatu
waliotokana na mahari za binti zangu wawili baada ya hapo masumbuko alianza
shule,masumbuko alikuwa na uwezo mkubwa sana darasani na kila siku za mwishoni
mwa juma(weekend) alikuwa anarudi nyumbani kutusaidia kazi za shamba na kuchunga
pia.
Ilikuwa ni siku moja ya
jumapili,kama kawaida yake masumbuko alikuwepo nyumbani kutusaidia kazi siku
hiyo alienda kuchunga na aliporudi hata kabla ya kula chakula cha usiku alinifuata
nilipokuwa nimekaa nikiwa naota moto pembezoni mwa zizi,masumbuko alionekana
anamawazo mengi sana na ilionyesha alikuwa na jambo lakunambia baada ya
kusisimama kwa muda alichukua gogo lilokuwepo jirani akakaa akaanza kuota moto
pia.
Vipi mwanangu nambie tu
unasumbuliwa na nini? nambie
Kusema ukweli baba mimi
sielewi hata nianzie wapi,nilipokuwa natoka kuchunga nikiwa nakaribia kwenye
shamba letu la mahindi nilisika sauti za wanawake wawili zinaniita hata
nilipogeuka sikuona mtu,baada ya kutoona mtu nikaamua kwendelea kuja nyumbani
lakini baada ya hatua kama 10 nilihisi kuna mtu alinishika mikono yangu hadi
nikashindwa kutembea ila ghafula nikasukumwa nikaanguka hadi nikachubuka hapa
mkononi
Pole mwanangu,tambua
ukimwona nyani mzee jua kakutana na mishale mingi,na sasa ndiyo unakua mwanangu
yote hayo yataisha usiwe na hofu,sawa?
Sawa baba
Niliamua kumtoa hofu
masumbuko lakini hofu kubwa nilikuwa nayo mimi sikutaka tena nianze kushuhudia
matukio ya kichawi maishani mwangu,tuliendelea kuota moto mimi na mwanangu
masumbuko hadi chakula kilipoletwa tukala pamoja ugali na maziwa na ulipofika
muda wa kwenda kulala tukaagana ila mimi hofu ilizidi kunitawala juu ya tukio
la mwanangu kuitwa na sauti za watu wasioonekana.
Nilijilaza kitandani
lakini usingizi haukupatikana maana mawazo niliyokuwa nayo ni juu ya
alichonieleza masumbuko mambo yaleyale yaliyonitesa mimi kwenye maisha yangu
niliwaza kwanini muda ule yalitaka kuanza kumsumbua mwanangu,kwa muda wote
usiku ulikuwa tulivu hadi ilipofika saa sita kuelekea saa saba kutokana na saa ya kwenye simu yangu ya nokia
tochi niliyokuwa nayo,kwa mbali sauti ya fisi ilisikika na kuwafanya mbwa wangu
wabweke kwa sauti kali kama kawaida ya kijijini mbwa wakibweka lazima kutoka
nje ya nyumba ili kuangalia kipi kinawasumbua mbwa maana unaweza kuendelea
kulala ukakuta ng`ombe wote wameibiwa au wameuliwa na fisi,nilijifunga rubega
kitenge cha mke wangu mkubwa maana siku ile nililala kwake nikachukua upinde na
mishale yakutosha na tochi ambayo ilikuwa na betri mpya kabisa nikatoka
nje,nilipokuwa pale nje naangalia usalama masumbuko naye alitoka akiwa na tochi
yake yenye mwanga mkali kuzidi tochi yangu na kwa upande wake alikuwa na panga
mkononi,mbwa walizidi kubweka wakiwa wanabweka kuelekea kwenye shamba
lenye mahindi jirani na zizi la
ng`ombe,moja kwa moja nikajua atakuwa fisi mwenye njaa anatafuta namna ya
kuingia kwenye zizi la ng`ombe,nikaichomooa mishale miwili yenye sumu
nikaiwekka sawa kwenye upinde kwa ujasilili mkubwa mimi na mwanangu masumbuko
tukaziwasha tochi zetu na kuelekea kule mbwa walipoelekea,tuliingia kwenye yale
mahindi kwa umakini tukawakuta mbwa
wamesimama mbali ya kichaka huku wakiwa wanabweka na macho yao yote yalikuwa
kwenye kile kichaka,huku tukitafakari ni kitu gani kitakuwepo kwenye kichaka na
namna gani tutashambulia pale tukiwa tunaendelea kupiga hatua kusogea sauti ya
mwanamke ikasikika kutoka kwenye kile kichaka na kwa haraka alisimama mwanamke akiwa
mtupu kabisa kama alivyozaliwa na kwa macho yangu nikamuona mke wangu mkubwa ambaye
ni mama yake masumbuko ambaye muda natoka ndani alikuwa anakoroma kabisa ila
masumbuko aliposhuhudia tukio lle alizima tochi kwa haraka…….………………………..INAENDELEA
Comments
Post a Comment