HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KUMI (10)
BABA MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook:Yahilima PM
SEHEMU YA KUMI (10 )
Baada ya tukio lile na
kumbaini kuwa aliyekuwa kwenye kile kichaka ni nani sote wawili tulizima tochi
zetu na kila mmoja akarudi nyumbani kwa njia aliyoijua yeye,masumbuko aliwahi
kufika nyumbani akaingia kwenye nyumba yake kabla mimi sijafika nyumbani,nilipofika
nyumbani nikawaza kipi nifanye lakini nikaamua liwalo na liwe nikaingia
chumbani kwangu,nikamkuta mke wangu mkubwa ambaye ni yule yule tuliyemwona
shambani akiwa kwenye hali ya ajabua ambayo nilishawahi kuiona gamboshi siku za
nyuma na hakuna mtu hata mmoja angebisha kuwa Yule si mchawi baada ya kuliona
tukio lile,nikaukaza moyo kiume nikalala pembeni yake lakini yeye aliendelea
kukoroma tu,mpaka inafika asubuhi sikuweza kupata usingizi hata kidogo hali ile
ilinifanya niwahi kutoka ndani kuliko mtu yoyote maana niliamka saa kumi na
moja asubuhi kabisa,nikiwa pale nje nikaanza weza kuzaa watoto wengine tofauti
na mke wangu mdogo ambaye hadi muda huo alikuwa amezaa watoto wa tano japo wote
ni wa kike.
Kulipokucha saubuhi
wake zangu wakaanza kukamua na baada ya kukamua walienda shambani,mimi sikuwa
hata na nguvu ya kwenda shambani nilibaki nyumbani hadi chakula cha mtu ambaye
alikuwa anaenda kuchunga kikapikwa na muda ulipofika wa kula niliitwa nikale
ila sikuwa na hamu ya kula kabisa nikaishia kunywa maziwa tu kisha nikarudi
chumbani kwa mke wangu mdogo nikajilaza kitandani nikitafakari mambo mbalimbali
yaliyotokea na haukupita muda mrefu usingizi ukanipitia,nilishituliwa kutoka
usingizini na mlio wa simu,ilikuwa ni namba ngeni nikaiangalia simu kwa muda
kisha nikapokea
Shikamoo baba mimi
masumbuko
Marhaba uko wapi?
Niko shuleni nilitoka
hapo nyumbani usiku ule ule.
Uko salama lakini, na
pia nakuomba tukutane kwa mganga wa kienyeji bwana ganungo ga walwa uwahi
sana sawa?
Haya baba
Baada ya maongezi hayo
mafupi furaha ilirudi maana nilijua mwanangu yuko hai,nikaanza kujiandaa kwenda
kwa mganga wetu bwana ganungo ga walwa amabaye kwa kifupi tulizoea kumuita
bwana ganungo nilimchukua beberu ambaye alikuwa mkubwa zaidi ya wote,beberu
ambaye harufu yake ilikuwa inawafanya watu wapone mafua kabisa,nilichukua jogoo
wawili na bata mmoja,lemgo langu kubwa lilikuwa ni kuenda kumwomba msamaha
kutokana na kutokuelewana kwangu na yeye hadi akataka niuliwe kule mlimani na
pia kumwoma anisaidie juu ya matatizo niliyokuwa nimekumbana nayo,nilitembea
kwa mwendo wa haraka hadi inafika saa 10 jioni nilikuwa nimeshafika kwa mganga,alinipokea
kwa furaha na kunipa maneno ya tumaini pia akanisihi hatotoa msamaha kwa kosa
jingine litakalojitokeza na akanisihi ili nifanikishe ninayoyataka ni lazima
niwe makini kwenye kutekeleza lolote ninaloagizwa bila kukiuka hata sharti
moja,tukiwa tunaendelea kuongea masumbuko akafika kwa pamoja tukaa sehemu moja
na mganga hadi usiku ulipoingia tukiwa bado hata hatujala chakula cha usiku mwanangu masumbuka alianguka chini akaanza
kutokwa na mapovu mdomoni huku akigaragara chini,mganga alikuwa kwenye nyumba
maalumu ya kufanyia tiba akaja akambeba masumbuko hadi kwenye ile nyumba ya
kutibia muda huo mimi sikuwa na nguvu ya kufanya lolote mwili wangu ulikuwa
unatokwa na jasho tu
Mganga alijitahidi kwa
kila namna kwa kubadilisha kila aina ya dawa lakini hakuna mabadiliko
yaliyonekana, aliongea lugha nyingi ambazo sikuzijua hata kidogo lakini hadi
saa tisa usiku mwanangu masumbuko aliamka akajipapasa vumbi kisha akaelezea
jambo jipya akidai muda uliopita alikuwa gamboshi kwenye mkutano,baada ya
maneno hayo kila mtu akawa kimya akitafakari ni wapi aanzie ,nilimtazama kwa
muda mwanangu nayeye akanitazama kisha akanionyesha tabasamu nililolizoea kisha
akanikumbusha mambo yaliyotokea kipindi akiwa mdogo sana ambayo mambo yale
sijawahi kumwambia mtu yoyote,aliniumbusha mambo yaliyotokea gamboshi kipindi
kile nikiwa nimekaa mbele ya kundi la wachawi kwenye ukumbi mkubwa sana ambao
sijawahi kuuona pengine popote siku ile nikiwa mbele pale mwanangu alilionekana
na mimi nikambeba kwenye mikono yangu kisha taa za mule zilizimika na
zilipowaka tena nilijikuta nimeshika joka.baada ya pale sote tulipitiwa na
usingizi lakini mtu mmoja ambaye simkumbuki alikuja akaniamsha na mimi nikamfuata
na muda huo ilikuwa ni asubuhi yule mtu alishika mkono nikamfuata hadi nyuma ya
nyumba moja kisha akakimbia kuelekea ndani
ya shamba la jirani na nyumbani kwa mganga nilipoangalia kwa makini nikaona
watu wengi wakikimbia kuelekea kwenye msitu mdogo na mimi nikazidi kukimbia ile
tu nakaribia nione kipi kimetokea na ni kipi watu wanakiangalia,macho yangu
yalimwona masumbuko akiwa amejinyonga kwa kamba ya katani baada ya hapo sikujua
kitu gani kiliendelea tena.
Baada ya muda
usiojulikana nilifumbua macho nikakutana na watu wengi pembeni yangu alikuwepo kuna
mzee mmoja wa makamo nilimuuliza kuna nini na yeye hakusita kunambia,aliniambia
hadithi yote ya yaliyotokea na ilikuwa ni siku ya tatu nikiwa nimepoteza fahamu
na nilipozinduka siku ile ndo siku ambayo mwanangu niliyempenda sana alikuwa
amezikwa kwa maana walnisubiri kama nitaamka lakini sikuamka ndipo wakamzika kwa
hiyo niliishiia kuliona kaburi tu,ilipopita wiki moja yule mganga alinambia
nimfate nyumbani kwake na mimi sikuona kama kuna tatizo nilitii wito wake,siku
hiyo mganga alikuwa anaonekana mwenye kufikili sana na alikuwa anaonyesha
kunihurumia sana.
Masanja kifulambute
hivi kweli unamjua mchawi anayekumaliza?
Ndiyo namjua ni mke
wangu mkubwa
Sasa wewe unadhani ni
njia gani ya kumaliza tatizo hili?
Mganga,mi nakuomba fanya
vyovyote afe kabisa
Mimi siwezi kuua ila
wewe ndiye uue maana huyo ni adui yako,utaweza au bado unampenda?
Maswali ya mganga
yaliibua hasira zaidi kwa mke wangu na nikaona dawa yake ni kuua tu,mganga
akanipa mashariti zaidi kuwa nikitaka kuua lazima niue ijumaa na ni lazima uwe
wakati wa kula chakula cha jioni,nikajipanga kutekeleza mauaji kwa kuandaa
panga mpya kabisa ambayo niliinoa kwenye mashine ya kunolea na mganga aliipaka
mafuta ya Baraka,siku ya ijumaa ikafika na muda wa kutekeleza kila nililopanga
ukazidi kusogea,ilipofika saa mbili usiku muda huo nilikuwa nimevaa nguo zangu
za kazi ambazo si rahisi mtu kunijua na kichwani nilivaa mask nyeusi kufunika
uso mzima tayari kabisa kumwondoa duniani mke wangu mkubwa,nikasogea taratibu
hadi karibu na nyumba ya mke wangu mkubwa na baada ya moshi uliokuwa unatoka
kwenye nyumba ndogo ambayo ndiyo jiko alimokuwa akipikia mke wangu nilianza
kunyata taratibu …………………………INAENDELEA
Comments
Post a Comment