HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NANE(8)



                                                           HADITHI YA
                                                          BABA MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook: Yahilima PM
                                                                 SEHEMU YA 8

Baada ya Yule mzee kuamuru nikamatwe,watu wawili wenye miili mikubwa walisimama kutokea nyuma ya lile kundi la wachawi wale jamaa wakaanza kuja kwa kasi sehemu nilipokuwa maana nilikuwa bado niko mbele ya ule ukumbi nilizidi kutetemeka kadiri walipokuwa wananikaribia nilipokuwa nimekaa sikuwa hata na nguvu ya kukimbia nikabaki palepale,walipofika nilipokuwa wakaninyanyua kwa nguvu na kuanza kuniburuta chini huku kila mmoja akiwa ameshika mkono mmoja mmoja,wakaendelea kunivuta  kama mzigo hadi kwa Yule mzee aliyekuwa anaonekana kuwa mkuu wao kisha wakaniachia nikakaa chini  mbele ya Yule mzee,muda wote nilikuwa natetemeka sana na jasho jingi lilikuwa linanitoka huku mapigo ya moyo niliyasikia yakipiga kwa kwa kasi isiyo ya kawaida,Yule mzee aliniangalia kwa makini kisha akaamka alipokuwa amekaa kisha akanisogelea na kuanza kunikagua sehemu za mwili wangu

Pimbi kasoro mkia wewe,umekiuka masharti

Nisamehe,sikujua

Ndugu wageni na wenyeji huyu kijana hapa amefanya kosa kubwa,nimemchunguza nimeona makubwa,kawaida yetu tukiwa tunakula huwa hatuli chakula kwa vijiko kama watu wajinga wa mitaani wala hatuli kwa viganja vyetu,kama mnavyojua sisi huwa tunakula kwa kutumia viganja vya watu vilivyokaushwa kwa moto wa mianzi  ila yeye amekula kwa kutumia viganja vyake ambavyo ni anasa kwa gamboshi na kwingine,na ni nani kamleta huyu humu hata kabla ya hii sherehe kuisha aondoke na aliyemwagiza kuja huku ndiye ataubeba msalaba wa huyu pimbi wake na mtoeni haraka asiendelee kututia anasa humu

Nisamehe,sitarudia

Baada ya maamuzi ya Yule mzee wale jamaa wawili wenye miili mikubwa walikuja tena wakaniangalia kwa muda kisha wakaniamuru niwafuate na mimi sikuwa na ubishi,wale jamaa walitembea huku mimi nikiwa nyuma yao hadi kwenye mlango mmoja,wakafumba macho nakuanza kuongea maneno nisiyoyajua baada ya muda mfupi ule mlango ukafunguka tukaingia wote mle ndani,kile chumba kilikuwa na giza sana na hewa ya mule ilikuwa nzito sana na mimi nilizidi kuwafuata wale watu,tulitembea hadi kwenye chumba kingine kile chumba kikafunguka chenyewe sote watatu tukaingia mle ndani tukamkuta jamaa mmoja mweusi sana,nikiwa bado natafakari jamaa tuliyemkuta kwenye kile chumba akaja akaniangalia kwa muda kisha akaanza kuongea na wale jamaa wawili nilioingia nao mle chumbani sikujua walichokuwa wanaongea kutokana na kutoijua lugha waliyokuwa wanaongea,baada ya mazungumzo ya muda mfupi Yule jamaa mweusi tuliyemkuta mle akapiga mruzi na baada ya sekunde chache nilimwona fisi niliyeenda naye usiku ule akiwa anakuja nilipo,alikuja hadi niliposimama,kisha wale jamaa wakaniamba niondoke haraka eneo lile na mimi sikuchelewa nikapanda mgongoni mwa Yule fisi nikafanya kila nilichoelekezwa na mganga wangu kuhusu namna ya kumwendesha yule fisi,hazikupita hata sekunde kumi nikaondoka na fisi Yule kwa kasi sana na  ndani ya dakika kama 20 kwa mbali nikaiona nyumba ya mganga aliyeniagiza,nilifika nyumbani kwa mganga hata kabla sijashuka kwenye fisi nikamwona mganga nje ya nyumba yake

Umefanya nini sasa,yaani umeniingiza kwenye matatizo

Lakini sikujua mashariti ya kule

Ujinga wako tu,na najutia kukuagiza wewe na kuanzia leo tusijuane

Mganga aliongea kwa hasira hata nilipokuwa namwomba msamaha hakunisikiliza kabisa na aliendelea kunitukana,Baada ya majibizano ya muda mrefu na mganga aliamua kunipa masharti mapya kabisa ili niweze kusafisha nyota yangu na nikiyakamilisha yale masharti atanipa dawa ya kuwa tajiri sikuwa na lakujitetea  nikasubiri ni masharti gani atanipa,ilipofika mida ya saa nane usiku mganga alitaka nimfuate na mimi nilimfuata hadi tukafika njia panda iliyokuwa jirani kabisa na bwawa kubwa la kijiji,baada ya muda mfupi tukiwa pale njia panda,mganga akaanza kuongea maneno yasiyojulikana huku akilia na kila mara jina langu alilisema likifatiwa na jina la gamboshi moyoni mwangu nikajawa na uoga nikajiuliza labda anataka kunirudisha  gamboshi tena nikaanza kufikilia kipi cha kufanya lakini nikiwa bado nafikilia mganga alikuja nilipokuwa akanishika kichwa kwa mkono wa kushoto kisha akanipiga kwa kitambaa cheusi alichokuwa nacho kwenye mkono wa kulia akiwa anaendelea kunipigapiga kwa kile kitambaa taratibu nguvu zilianza kuniishia na macho nayo  yakaanza kujawa na usingizi  hata sikujua ni wapi  usingizi huo ulitokea ila badaye nilipofumbua macho nilijikuta nikiwa sehemu ambayo sikuitambua kwa mara moja na wakati huo sikuona hata mtu mmoja na sikuona chakunisaidia huku hofu ikiwa inazidi kunipata ,hofu iliyosindikizwa na baridi kali sikutaka kuwa mzembe nikaamua kusimama,taratibu nikavuta pumzi ndefu kisha nikasimama ndipo nilipojua kuwa nilikuwa kwenye mlima uliopo karibu na kijiji chetu na huo mlima unaogopesha sana hasa mida ya usiku maana wachawi huwa wanakutana kwenye huo mlima na mara kwa mara moto huonekana kwenye ule mlima mida ya usiku,nikiwa naendelea kufikilia nifanyeje nikahisi kama kuna mtu ananipuliza kwenye sikio la kulia nikageuka lakini sikouna chochote,sikutaka kupoteza muda nikaamua nishuke kwenye mlima lakini kila nilipokuwa najaribu kutembea nilijikuta niko palepale nikajaribu kukimbia lakini nikawa palepale hata nilipojaribu kukaa sikuweza tena nikahisi kama kuna watu wananishikilia ili nisikae,baada ya dakika kama 30 nilisikia vishindo vya watu vinanizunguka kisha ukimya ukatawala sikujua kipi chakufanya ikanibidi niwe mpole tu

Ahahahahahaha nimempata vipi mmemwona?

Tumemwonaaaaaaa

Je,anatufaa au hatufai?

Anatufaaaaa!

Sauti za watu zikasikika karibu na nilipokuwa nimesimama na baada tu ya zile sauti mwanga uliwashwa kutoka kwenye mwenge waliobeba wale watu,hawakuwa watu wa kawaida walikuwa ni wafupi sana akili ikanituma kuwa wale ndo ambao huitwa vibwengo na hata baada ya kuwepo kwa mwanga pale ukimya uliendelea kuwepo wakati huo wale watu wafupi walikuwa wamenizunguka ,mawazo yalinijaa nikiwa nawaza nifanyeje nilishitukia kofi zito likitua kwenye shavu langu la kulia na nilipogeuka nikamkuta mganga kisha akacheka kicheko kikubwa ambacho kiliniudhi sana nikamtemea mate mganga lakini hakuonesha chuki yoyote akacheka tena kisha akawaamuru wale watu wake waondoke,sikujua waliondokaje pale maana ndani ya sekunde kama tano walikuwa hawaonekani tena na walipoondoka tu ukimya ukatanda na giza kubwa liliufunika mlima ule,mganga akajikoholesha kidogo kisha akaliita jina langu kutokana na hasira sikuitika na baada ya kuona kuwa simwitikii na nina hasira akanisogelea akanishika mkono wangu wa kulia kisha akaanza kuongea maneno yake nisiyoyajua na baada  ya kumaliza kuongea maneno yake ya ajabu kila alichoniamuru nifanye  sikutii ila hakukata tamaa akaanza kunipa masharti ili niweze kusamehewa na niweze kusafisha nyota,sharti lake la  kwanza alitaka nimtoe kafara mtu ninayempenda ili nyota yangu iwe safi na nikishatoa kafara nitakuwa tajiri,bila kupoteza muda nilimchagua mtoto wangu wa kwanza wa kike kutoka kwa mke wangu mdogo lakini baada ya kumweleza hilo alinitukana sikujua kwanini kisha akadai nimchague mwingine na mimi nikamchagua  Yule mtoto wa kike wa pili wa mke wangu mdogo ila aliachia msonyo mkubwa kisha akanitukana sana akadai kuwa mizimu haipendi kafara ya watoto wa kike ila inapenda watoto wa kiume sana hivyo akaniambia nimtoe mtoto wangu wa kiume ambaye ni wa pekee tuliyempa jina la masumbuko mwanangu ambaye sikuwahi kulifikilia kuja kumfanyia unyama licha ya ahadi za utajiri na kusafisha nyota nilikataa katakata kumtoa kafara mwanangu huku machozi yakiwa yananitoka,Baada ya maamuzi yangu mganga alienda pembeni akakaa akaanza kuongea na watu ambao sikuwaona ila nilizisikia sauti tu muda huo roho ya ujasili ikaniingia na nikaanza kupiga hatua ili nitoroke ila nilipoanza tu kutoroka  kwenye ule mlima hata kabla sijafika mbali walau nikaribie nusu ya mlima niweze kushuka chini nilisikia sauti ya mganga ikiamuru nikamatwe na nikisumbua waniue nikajiuliza kipi chakufanya na nikakiona kifo kinanikaribia....................INAENDELEA
                                                                                                            

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KWANZA (1)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)