HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA SABA (7)
HADITHI YA
BABA MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook:Yahilima PM
SEHEMU
YA SABA
Baada ya kumwona nesi akiwa mwenye
haraka na uoga mkubwa akiwa anatoka kwenye wodi huku akiomba msaada sikutaka
kupoteza muda nikasimama kwa haraka nikaingia ndani ya ile wodi ambamo mgonjwa
pekee aliyekuwemo ni mke wangu tu,nilipoingia kwenye ile wodi nilichokikuta
kilikuwa cha hatari,nilikuta bundi wengi sana kwenye ile wodi wakiwa
wamekizunguka kitanda alicholalalia mke wangu hali ya uoga ilikuwa imenijaa
moyoni mwangu,roho ya ujasili iliniingia nikanza kupiga hatua kwenda kwenye
kitanda alicholazwa mke wangu ila nilipokaribia tu wale bundi wote wakapotea na sikujua ni
njia gani walikuwa wameingilia na walipotokea,nilishikwa na mshangao sana
kilichonishitua na kunitoa kwenye maazo ni sauti ya nesi alikuwa anakuja
ameambatana na Dokta
Dokta,yaani niliyoyaona ni
ya hatari?
Wewe acha uongo,kuwa na moyo
mgumu
Yaani nilipokuwa naanza kumsaidia
ili ajifungue kuna mtu alininong`oneza eti mtoto akizaliwa nimuue na nikiwa natafakari walitokea
bundi wengi na sijui walitokea wapi ndipo nikatoka nje kuomba msaada
Pole sana lakini ndiyo kazi
Yule nesi na dokta wa zamu ya
asubuhi waliingia wakanikuta ndani ya wodi wakaniuliza kama kuna kitu nimeona
ila nikasema sijaona ili kuwapa moyo waweze kumsaidia mke wangu ambaye muda huo
alikuwa anajirusha rusha tu pale kitandani,baada ya hapo waliniambia niwapishe
na mimi nikawapisha nikaenda nje nikakaa kwenye benchi nililokaa mwanzo
Baada ya masaa kama matatu nesi
alikuja akiwa mwenye furaha sana akanichangamkia tofauti kabisa na wauguzi
wengine ambavyo huwa wanafanya,aliniita jina langu na mimi nikaitika kisha
akanambia nimfuate na mimi sikuwa na
ubishi wowote nikamfuata kwa nyuma,tulipita vyumba vingi kisha akaingia kwenye
chumba kimoja na mimi nikaingia,kilikuwa
ni chumba kizuri ndani ya kile chumba kulikuwepo meza na viti viwili,kiti
kimoja upande mmoja wa meza na kingine upande wa pili,Yule nesi alikaa upande
mmoja kisha akanikaribisha huku kichwani kwangu nikiwa na mawazo mengi kama mke
wangu alipo ni atakuwa salama au vipi
Nesi,usinifiche we nambie hali ya
mke wangu
Mmh! Haraka ya nini na uko kwenye
huduma hapa
Nambie kama mke wangu kajifungua
salama au laa na kama bado nambie
Mkeo yuko salama,nimekuita
nikupongeze kwa mkeo na umri wake huo kupata mtoto ila sikwambii kama ni wa
kike au kiume
Baada ya kuambiwa kuwa amejifungua
salama nilifurahi kisha nesi akaniambia nimfuate na mimi sikuwa na jinsi nikamfuata,tukaingia
kwenye wodi alimolazwa mke wangu tukamkuta amesinzia,nesi hakutaka kumsumbua
akamchukua Yule mtoto,nilifurahi sana kuona ni mtoto wa kiume japo ni mdogo
tena hata siku hajamaliza ila alikuwa anafanana na mimi kabisa.Baada ya huduma
nzuri za kwenye ile zahanati na wauguzi kutuaga,niliondoka
na mke wangu mkubwa ambaye tokea nioane naye ni mwaka wa 12 ndiyo amefanikiwa
kunipatia mtoto wa kiume,hakika nilikuwa nafuraha sana muda wote na mapenzi
yalikuwa yamerudi kwake,sikutaka kuwa mbali naye na lengo kuu ni kumwona mtoto
wangu wa kiume akikuwa kwa malezi bora kabisa ilifika kipindi mke wangu mdogo
hakupata tena hata nafasi ya kumuwaza hata hela ya matumizi ikawa kila mara napeleka
kwa mke mkubwa nilikuwa naleta matumizi kama sabuni,nguo na mboga kwa mke
mkubwa hali iliyomchukiza sana mke wangu mdogo tena kwa chuki za wazi wazi ila
hilo sikulijali hata kidogo
Miezi miwili badaye niliamua niende
kwa mganga wangu wa kienyeji ili nikatafute dawa ya kujikinga mimi mwenyewe na
mwanangu wa kiume,niliandaa vitu vya kwenda navyo kwa mganga nilibeba jogoo
wawili weusi na beberu wawili mmoja mweusi mwingine mweupe ambaye hakuwa na doa
lolote.nilifika kwa mida ya jioni nikamkuta mganga na watu wengine na baada ya chakula cha jioni alinipa
maelezo kuwa mimi ni mkosefu tokea kipindi nilipokataa kupelekwa Mombasa na
wale jamaa wawili kwa hiyo ili nisamehewe kosa langu ni lazima nikubali kutumwa
na mimi sikuwa mbishi nikakubali kutumwa alipotaka,mganga akanipa ngozi ya
mnyama ambaye sikujua ni mnyama gani kisha akaniamuru nivue nguo zote na mimi
nikafanya kama alivyotaka, baada ya kuvua nguo zangu zote mganga akanifunga kiunoni
ile ngozi kama watu wa zamani au wa polini maarufu kama bush man,baada ya hapo
akanimwagia maji ambayo yalikuwa na harufu mbaya sana na mengine akanambia
ninywe na mimi nikafanya kama nilivyoagizwa.
Ilipofika saa tano usiku akaniita
nimfuate na mimi nikamfuata hadi kwenye
chumba kimoja tukaingia wote kisha
akatoa dawa ya unga yenye rangi nyeusi akaniambia nifumbe macho kisha akazipaka
nyusi zangu hadi akamaliza kuzipaka alipomaliza
tu akanambia nifumbue macho,niliogopa sana nilipofumbua macho tu nikajikuta
katikati ya fisi wengi lakini mganga alipoona nimeogopa akanichoma kwa kitu
chenye ncha kali kama sindano,damu ilitoka kidogo naye akaikinga kwenye upembe
wa swala kisha akachanganya na dawa fulani nyekundu akajiongelesha maneno
ambayo sikuyaelewa baada ya kitendo hicho akaniamuru ninywe ile dawa iliyochanganywa
na damu baada ya kunywa tu ile dawa hofu juu ya wale fisi ikatoweka nikawa
nawaona kama mbwa tu,mganga akaniamuru nichague fisi ninayemtaka na kwa ujasili
nikachukua fisi aliyekuwa mkubwa zaidi ya wenzake,mganga alicheka kwa sauti
kubwa kisha akaendelea kunipa maelezo mengine nikiwa nimepanda juu ya Yule fisi
Shika masikio hayo vizuri,ukitaka
kona ya kulia minya hilo sikio la kulia na ukitaka kona ya kushoto minya sikio
la kushoto na kuongeza spidi shika mkia pia usiongee njia nzima wala usitazame nyuma,umeelewa?
Ndiyo nimeelewa mganga
Safari njema na leo najua ni mara
yako kwanza utaiona gamboshi,kumbuka ukiona wanawake wazuri wakiwa uchi uendako
tafadhali kidudu chako kisiwe na kihelehele cha kusimama watakikata
Nilianza safari mida ya saa tano hivi
lakini ndani ya dakika kama 20 nilikuwa tayari niko gamboshi,nilipofika
nilipokelewa kwa shangwe na nikajiuliza kama huo mji uko Afrika au wapi maana
sijawahi kuuona hata kwenye picha,siku hiyo ndipo nilipojua kwanini unaweza
kulala ukaamka umechoka sana,nilichokiona ni kuwa kule hakuna viti ila watu
huwa wanaenda kuamshwa majumbani mwao kichawi bila kujua wanaenda
kutumikishwa,walikuwepo watu wengi wameinamishwa kisha migongo yao kufanywa
kama viti na wachawi,wageni walizidi kuingia na wengi walikuwa wanajuana,mimi
nilipofika nikaona si vizuri kukaa kwenye migongo ya watu nikaamua kukaa chini
maana niliangalia popote sikuona
kiti,nikiwa bado naangalia mazingira kuna watu wawili walikuja karibu na mimi
na mimi nikawatambua vizuri kuwa ni wale watu waliofukua maiti ya mwanangu siku
za nyuma,nikiwa bado nawashangaa wale watu sauti kubwa iliita jina langu kwa ufasaha nikajiuliza nani anayefahamu hapo
Masanja kifula mbute
Naam!
Wewe ni mgeni lakini mjinga au
unataka ushindwe kupeleka ulichoagizwa kwa aliyekuagiza
Nisamehe sana
Nikaitwa nipite mbele ya ukumbi ule
nikapita mbele kisha wakaletwa watu wawili wakainamishwa nikaamuriwa kukaa na
mimi nikafata amri baada ya kukaa ukumbi mzima ulinipigia makofi na baadaye
ukawa kimya yaani ule ukimya ambao ukiangusha sindano unaweza kusikia kishindo
chake,na mimi sikuwa na jinsi
nikatulia,baada ya dakika kama mbili kutoka kwenye upande mmoja wa ule
ukumbi lilitokea joka kubwa ambalo sikuwahi kuliona maishani kwangu,lile joka
likatambaa taratibu hadi sehemu nilipokuwa huku mapigo yangu ya moyo yakiwa
yanaenda mbio sana,lile joka likatoa ulimi likiwa linataka kunimeza na mimi
nikafumba macho kusubiri kinachofuata lakini sikuona wala kuhisi chochote kinachotokea,nilifumbua
macho taratibu kwa uoga nilipofungua macho yote mbele yangu nikamwona mwanangu
wakiume ambaye tulimwita masumbuko akiwa kando yangu na nilipoangaza macho
sikuona mtu yoyote kwenye ule ukumbi
mwanangu alianza kulia pale pembeni nikamwonea huruma mwanangu masumbuko,nikapeleka
mkono ili nimbebe ile tu nasogeza mkono giza likatanda kwenye ule ukumbi
nikajitahid hadi nikambeba mwanangu baada ya kumbeba nikaaamka taratibu kupapasa kwenye ule ukuta wa ule ukumbi ila
kadili nilivyozidi kuupapasa ule ukuta ulizidi kuwa mbichi,mwanangu masumbuko
nilimshika vizuri kwa mkono wa kulia
huku mkono wa kushoto ukiwa unapapasa nikitafta njia ya kutokea,nikiwa
naendelea na lile zoezi la kupapasa tena kwenye giza kelele za shangwe
zilisikika hapo hapo mwanga ukarudi na wale watu waliokuwemo mwanzoni wakawemo
wote na nilipomangalia mwanangu sikumwona tena nilikuwa nimebeba joka lile
kubwa,kwa uoga nikalitupa chini lilipotua tu chini likabadilika akawa ni
mwanangu sikutaka tena kumfata ikanibidi
nirudi nilipokuwa mwanzo pale mbele ya ukumbi nikarudi nikakaa tena kwenye ile
migongo ya watu walioinamishwa
Mpeni chakula ale,anaonekana ana
njaa
Nimeshiba! Mimi sina njaa
Kwa hiyo hutaki chakula chetu
Nataka! Nipeni nile
Walileta chakula cha kila aina
mwanzoni nilikataa kula ili niepushe mgogoro ikabidi nile tu,baada ya kula hakukuwa
na maji ya kunawa wala maji ya kunywa ila watu walikunywa vitu nisivyovijua na
mimi nililetewa nikanywa kilikuwa ni kinywaji ambacho hakikuwa na utamu wowote
na hakikuwa na hakikuwa na uchungu wowote,watu wote walimaliza kula na kunywa
kwenye lile kundi alikuwepo mzee mmoja ambaye alionekana ni mkuu zaidi ya wote
aliamuru watu wote watulie na wote wakatulia kukawa kimya kabisa mle ndani na baada
ya ukimya kidogo Yule mzee ambaye
alikuwa anaonekana kuwa kiongozi wao aliamuru nikamatwe akidai nimekiuka masharti
ya gamboshi……………ITAENDELEA
Comments
Post a Comment