HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA SITA (6)
HADITHI YA
BABA MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
Facebook Yahilima PM
SEHEMU YA SITA
Nikiwa bado nipo kwenye mshangao wa
kumwangalia yule mtu aliyenigusa mgongoni akatoa rungu kisha akanipiga rungu
kichwani kisha akaniamuru nnyoshe mikono juu na mimi nikatii nikanyosha.yule
mtu alikuwa ni askari polisi nikiwa bado palepale nikisikilizia maumivu
kutokana na rungu niliyopigwa kichwani mabomu ya kutoa machozi yakaanza
kusikika na kelele za watu zikawa zinasikika kila sehemu nikajua kuwa askari wa
kikosi cha kuzuia ghasia watakuwa wamefika,Yule askari aliyenigusa mgongoni na
kunipiga rungu akaniamuru ninyoshe mikono kwa nyuma kisha akatoa pingu akanifunga
mikono yote kwa nyuma akaniamuru nitembee kuelekea alipotaka yeye na mimi
nikafata kile alichoagiza,tukafika mpaka kwenye gari la polisi akaniamuru
niingie kwenye lile gari nikafanya kama alivyoniamuru,Yule askari akapanda
kwenye lile gari akasimama na mimi nikakaa huku nikiwa nimeegemea ukuta wa lile
gari la wazi la polisi,kwa muda kama wa dakika 30 milindimo ya mabomu ya kutoa
machozi ilitulia,Nikaanza kuwaona askari wengi wakiwa wanarudi kwenye magari
yao,
Oyaa makamanda twendeni,hawa wasenge wameua makamanda wetu
wawili nasisi tumewaua watatu
Twendeni tukajipange turudi tena
Askari waliingia kwenye magari yao wakaanza kuondoka na baadhi
ya askari waliponiona mimi ndani ya lile gari walijawa na hasira sana,kimya
kimya nikamwomba mungu anisaidie ili nisije geuzwa mbuzi wa kafara maana ndiye
mwanakijij pekee niliyekamatwa,ilikuwa ni mida kama ya saa10 alfajili wale
askari wakaanza kuelezana kitu ambacho sikukisikia ila nilihisi ni jambo la
hatari walikuwa wanalipanga juu yangu na baada tu ya kuvuka mto unaotenganisha
kijiji chetu na cha jirani magari ya polisi ambayo yalikuwa mawili
yalisimamishwa na askari wote wakashuka baada ya muda kidogo askari mmoja kati
ya wale askari aliyeonekana mwenye hasira alitaka aniue ili alipize kisasi
maana askari wawili waliouliwa kwa kupigwa mishale na wananchi wote walikuwa
rafiki zake,lakini askari aliyeonekana kuwa mkuu wao alikataa nisiuliwe ila
akapendekeza nipewe mateso makali mpaka nitoe maelezo ya nani ni kiongozi wa
kundi lile ambalo limetekeleza mauaji ya askari na kuchoma nyumba,askari wawili
waliagizwa wakaja kwa haraka wakanibeba kwa mfumo unaojulikana kama Tanganyika
jeki,nilibebwa juu juu hadi nikafika katikati ya wale askari kwa haraka wakanizunguka na kuniweka kati,bila kuchelewa
wakanifungua ile pingu nikabaki nimesimama,lakini amri ikatolewa nipige magoti
na ninyoshe mikono juu nikiwa bado natafakari nikapigwa kitako cha bunduki
kichwani nikaanguka nikalala chali,licha ya maumivu makali niliyoyapata kwenye
kichwa baada ya kupigwa kitako cha bunduki niliendelea kuona na kusikia kitu
chochote kilichokuwa kinaendelea.
Yule kiongozi wa wale askari alikuja akaanza kunivua suruali
na alipohakikisha kuwa sina nguo hata moja akatoa mpira wa kufungia mizigo
kwenye baiskeli akaukata kipande chembanba hadi ukawa mdogo mdogo kisha akaanza
kunifunga kwenye sehemu zangu za sili,kwa ustadi akafunga yale mayai mawili
kwenye sehemu imayotenganisha mayai na shingo,katika maisha yangu sikuwahi
kupata maumivu makali kama niliyoyapata siku ile na sidhani kama nitayapata
tena siku nyingine,nilianza kulia kama mtoto mdogo,na askari wote walianza kunicheka
sana,macho yaliangaza pote lakini sikupata hata mmoja wa kunihurumia ila tu
waliendelea kunicheka.
Nikiwa bado niko kwenye maumivu yale,Yule mkuu wa askari
akaloweka kitambaa kwenye maji yaliyokuwa kwenye kopo dogo,kisha akaja
akanigusa kwenye sehemu waliyonifunga kwa kutumia ule mpira,hakika nilizidisha kilio zaidi ya awali kile
kitambaa kilikuwa kimewekwa kwenye maji yenye mchanganyko wa
pilipili,niliendelea kulia sana huku wakirudia kile kitendo cha kuniwekea maji
yenye pilipili,walipohakikisha kuwa nimelainika wakaanza kunihoji na kutokana
na maumivu niliyokuwa naendelea kuyapata nilieleza kila kitu na nilijitetea
kuwa mimi sina hatia lakini hawakunielewa, baada ya hunihoji wakanimwagia maji ya
baridi kisha wakanifungulia ule mpira walipomaliza wakanivalisha nguo na wakanifunga
pingu tena na kunitupia kwenye gari
Mkuu,sasa tunampeleka wapi huyu mbwa?
Huyu lazima akasadie upelelezi,pumbafu zake,
Askari wakapanda tena kwenye magari yao kisha wakaanza
safari kuelekea walipokuwa wanapajua wao ,kwenye maisha yangu nilikuwa muoga
sana wa polisi lakini siku ile muoga nilikuwa nimekamatika na sikuwa na namna yakufanya,gari zilianza
kwenda mwendo wa taratibu kutokana na ubovu wa barabara za vumbi zenye mabonde
mengi yaliyosababishwa na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha kwa wakati ule
lakini Baada ya mwendo kama wa kilomita moja tulifika sehemu ya
tambarale,dereva wa gali ambalo nilikuwepo mimi ambalo ndiyo lilikuwa liko mbele akazidi kuongeza
mwendo na muda huo jua lilikuwa limeshachomoza zamani ilikuwa ni mida kama ya
saa tatu asubuhi,gari niliyokuwemo mimi ilizidisha
mwendo kutokana na utambarale wa barabara,dereva alizidisha mwendo na wale
askari walianza kumshangilia sana kwa utaalamu wake wa kuendeha gari,sikujua
kipi kilitokea mbeleni ila nilisikia milio ya wale askari wengine walisema
“mungu wangu” na wengine walisema “mama yangu” hata sekunde tatu hazikupita
nilisika sauti ya mlipuko mkubwa na badaye sikujua ni nini kilifuatia maana
giza lilijaa machoni nikawa sikumbuki chochote.
Giza kiliendelea kutanda na sikuelewa chochote kwa muda
ambao sikujua ni siku ngapi zilipita,ghafula nilifungua macho na kujikuta
nimelala kwenye kitanda na nilipojaribu kuvuta kumbukumbu sikujua kuwa nilikuwa
wapi muda huo,macho yaliangaza pande zote lakini sikujua kuwa niko
wapi,nilijaribu kuinuka pale kitandani lakini maumivu ya mguu na mkono
yalinifanya nirudi kulala,nilianza kufikilia kama niko kwenye ndoto lakini kila
nilipojaribu kuamka,mguu wa kushoto na mkono wa kushoto vyote viliuma,ilianza
kufikilia nini kilitokea ndipo nikakumbuka kilichotokea na machozi yalianza
kunitoka ila hofu kubwa ilikuwa najiuliza ni wapi nilipo na ni nani kanileta
hapo,chumba nilichokuwa nimelazwa kilikuwa ni chumba chakavu kilichoezekwa kwa
mabati yaliyochoka sana na kuta za nyumba zilikuwa ni ya tope ila ilikuwa imepigwa
chokaa,nikiwa ndani ya fikra zile alikuja mtu ambaye namfahamu kabisa na
nilipomwona niliogopa na sikuwa na amani kabisa moyoni
Wewe mwanamke mchawi,usiyezaa muuaji umeshanichukua msukule
eti?
Mume wangu,tokea lini mimi mkeo nikawa mchawi?
Unafikili sijui Eti?,nirudishe kwa wanangu
Mume wangu sikia,wanasema tenda wema uende zako usisubiri
shukrani,mimi nimetenda wema kwa kukutorosha kule hospitali ukiwa umefungwa
pingu ukituhumiwa kwa ugaidi,unatuhumiwa wewe kuwa na kikundi cha watu
wanaopingana na serikali na siku ile ulipokuwa umekamatwa na polisi inasemekana
wenzako walitega bomu barabarani ndilo liliripuka hadi likafanya wewe upoteze
fahamu na uvunjke mguu na mkono,baada ya hapo walitaka wakuchome sindano ya
sumu ili ufe hata kabla hujapata fahamu kwani ni askari wengi walikufa kwenye
mlipuko uliotokana na bomu kutegwa barabarani lakini habari nilizipata
nikakutorosha na sasa uko kwa mjomba wangu huku lamadi
Mimi siyo gaidi waambie
Mke wangu alinieleza mambo
mengi alinieleza kuwa siku ambayo askari walikuja kule kijijini muda
ambao wanakijiji walitaka kuwaadhibu yeye na mama mkwe baada ya mimi kuzikata
kamba walizokuwa wamefungiwa mke wangu na mama mkwe waliwea kutoroka bila
kuonwa na polisi na wanakijiji kisha wakaenda hadi kijiji cha jirani,hata hali
yangu iliporudi kuwa kawaida yaani nilipopona niliendelea kuishi pale kwa mjomb
wake mke wangu wa kwanza,kwa muda wa miezi mitano nilikuwa mzima kabisa na
mwezi uliofuata mke wangu mkubwa aliniambia jambo ambalo lilinishitua sana na
sikudhani kama ingewezekana,aliniamia kuwa anaujauzito jambo ambalo
sikulikubali kwa maana nimeishi naye kwa miaka 12 lakini hakuweza kupata
ujauzito hadi ikanilazimu nioe mke wa pili ambaye amenizalia watoto wawili wa
kike na wa kiume ambaye alifariki siku ile anazaliwa,ilikuwa ni ngumu kumwamini
licha ya kuwa nilikuwa nashiriki naye tendo la ndoa kila mara tokea nipone mguu
na mkono kutokana na bomu kwa sababu kitanda hakizai haramu ikabidi nikubali
hali tu,
Niliendelea kuish kwa mjomba wake mke wangu,siku moja nikiwa
nasikiliza redio nikasikia kuwa polisi na wananchi wa kijiji changu kilichopo
kwenye mkoa wa simiyu kijiji cha matongo walipanga kwenda kufanya mapatano na
hata mimi walisema popote nilipo kama niko hai au nimeshakufa kuwa baada ya
uchunguzi imebainika kuwa sina hatia na hivyo popote pale nilipo niweze kwenda
hadi kijiji mimi pamoja na wake zangu ili tukaanze maisha mapya,nilipomweleza
mke wangu akawa na hofu sana akidhani kuwa utakuwa mtego ili nikakamatwe lakini
nilimsihi naye akakubali.Mjomba wa mke wangu alituruhusu kisha mimi na mke
wangu tulijipanga kwa safari,siku ya safari ilifika tukasafiri hadi tukafika
kijijini hakuna mwanakijiji aliyeonyesha chuki juu yetu,majirani walitusaidia
kujenga nyumba yetu hadi tukamaliza,viongozi wa serikali nao walikuja wakafanya mapatano na wanakijiji
na amani ikarudi tena
Mke wangu alilea mimba aliyoipata
hadi siku ya kujifungua ambapo matatizo mapya yalijitokeza,ilikuwa ni mida kama
ya saa saba usiku hivi ndipo mke wangu alipatwa na uchungu kabla ya kumpeleka
hospitali niliamua nimtafute mwanamke wa kumwangalia wakati mimi naenda kutafuta
pikipiki ya kutusafirisha hadi kwenye kituo cha afya,nilimwamsha mke wangu
mdogo amsaidie mwenzake lakini hakukubali sikuwa na jinsi nikaondoka kwenda kutafuta
usafiri,baada ya kurudi nilimkuta mke wangu mkubwa anatokwa na damu nyingi sana
mdomoni na puani na alikuwa tayari amepoteza fahamu,nilimsafisha damu mke wangu
nikambeba nikamuweka kwenye pikipiki kisha mimi nikakaa nyuma yake baada ya
kukaa sawa dereva akaanza safari,ila kadri tulivyozidi kusogea mbele milio ya
fisi ilizidi kusika kule tulipokuwa tunaelekea,baada ya dakika kama ishirini,kwa
mbali niliona kundi la watu ambao walikuwa wako uchi walipoona tunakaribia
walisimama katikati ya barabara sehemu
ambayo ilikuwa ni lazima tupite lakini dereva ilionekana aliwaona hakuweza
kupunguza mwendo ila alizidi kuendesha kwa mwendo wa kasi ili kunusuru maisha ya mke wangu mkubwa ambaye
alikuwa bado amepoteza fahamu,tulipokaribia pale walipokuwa wamesimama wale
watu kwa haraka waligawanyika pande mbili wakaachia nafasi ya barabara bila
kuwa na uoga derea akapita kwa kasi sana,tulipovuka pale nilisikia sauti ya
kike ikiita jina langu “masaja kifula mbuteeee” sikutaka kutazama nyuma wala
kuitika maana nilipokuwa kijana mdogo babu yangu aliniambia kuwa ukiitwa na mtu usiku maeneo usiyoyajua
usiitike wala kuangalia nani anayekuita,nilizingatia maelezo hayo ya babu na
sikuitika wala sikugeuka nyuma ila kadri tulivyozidi kwenya mbele sauti za fisi
zilizidi kusikika kutokana na sauti hizo
kuwa karibu yetu ilibidi nigeuze kichwa niangalie,hakika sijawahi kuona fisi
wengi kama wale maana nilizoea kuona fisi mmoja mmoja lakini kwa kukadiria wale
fisi walikuwa kama 25 hivi,nilishituka baada ya kuona fisi wale hadi dereva wa
pikipiki naye akageuza shingo na kuwaona wale fisi hali ile ilimlazimu kuongeza
mwendo maana bora uliwe na chui au simba kuliko kuliwa na fisi,chakushukuru baada
ya muda milio ya fisi ilianza kusikika kwa mbali.
Tulifika kwenye kituo kidogo cha
afya katika kijiji cha jirani cha sapiwi mkoani simiyu kwa bahati nzuri
tukamkuta nesi wa zamu ya
usiku,nikamlipa Yule bodaboda hela yake mimi nikamwingiza mke wangu kwenye wodi,akawekewa
dripu mbili za maji ndipo fahamu zikamrudia,niliendelea kukaa pale na mke wangu
na muda ule uchungu haukuwepo tena hadi ilipofikika saa kumi na mbili asubuhi
ndio uchungu ukaanza tena.
Kaka naomba upishe kidogo ili
nimsaidie mkeo
Haya dada,msaidie mke wangu
Usijali kaka ndo kazi zetu
Nilitoka nje ya wodi nikakaa kwenye
benchi moja pale nje,nilikaa kwa muda kama wa saa moja lakini sikumwona nesi
kutoka nje hadi nikawa na mashaka,ila muda natafakari juu ya hayo nesi akatoka
akasema nisiwe na wasiwasi maana mke wangu alikuwa anaendelea vizuri,nesi
alirudi kwenye ile wodi tena baada ya dakika kama 15 na mimi kutokana na uchovu
nikajikuta nimepitiwa na usingizi,nilishituliwa kutoka kwenye usingizi na
kelele za nesi kwani alitoka ndani ya wodi alimolazwa mke wangu,kelele za nesi
zilikuwa za kuomba msaada,gloves alizokuwa amevaa mikononi zilikuwa zimejaa
damu,alitoka mbio akanipita pale akaelekea nje huku akizidi kuomba msaada…………..INAENDELEA
Comments
Post a Comment