HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA PILI(2)



                                                                         HADITHI YA
                                                                          BABA MASUMBUKO
Mwandishi:PAUL M,YAHILIMA
0788624797
0765084515
Facebook Yahilima PM
Tembelea blog yake http://mla-ukoko.blogspot.com upate mwendelezo wa hadithi

                                                                          SEHEMU YA PILI
 Mke wangu alipozimia nilipata hofu kubwa sana maana nilijua kuwa nimemuua, mawazo mengi niliyawaza kwa muda mfupi, jambo la kwanza niliwaza kutoroka ila nikaoina ni jambo gumu maana ningetoroka familia yangu hasa mke wangu mdogo ningemwachia matatizo,niliamua kutoka nje ndipo nikapata wazo la kumpeleka hospitalini ikiwa atakuwa mzima au amekufa sikujali niliamua kubeba msalaba wowote utakaonifuata,ikanibidi kwa haraka niende  kwa mabula ambaye ni mtoto wa mjomba wangu ambaye ndiye pekee mwenye pikipiki kwenye sehemu ninayoishi,kwa kuwa ilikuwa ni usiku nilimkuta amelala nikamwamsha kisha nikamwelezea mkasa mzima na kwa haraka alinielewa tukatoka hadi nyumbani kwangu,haukuoita  muda sana jogoo akawika jambo hilo lilifanya nitambue kuwa ni saa9 au saa10,tukamchukua kwenye pikipiki ili kumpeleka kwenye zahanati ya kijiji cha sapiwi ambacho ni kijiji cha jirani kwa maana kijijini kwetu hakukuwa na kituo cha afya tulifika mpaka kwenye mto unaotenganisha jijiji chetu na cha jirani ambako haswa nilikuwa nampeleka akapatiwe tiba, tukakuta maji yamepungua sana kwenye mto tukafanikiwa kuvuka lakini tulipokariba kwenye zahanati mwenye pikipiki akakataa kwenda na mimi hadi kwenye ile zahanati  maana aliogopa kuingia kwenye kesi,kwa hiyo ikanilazimu kumbeba mke wangu mgongoni hadi kwenye zahanati hiyo na muda wote huo alikuwa amezimia,tulipofika kwa bahati nzuri tulimkuta nesi nikamweleza kuwa mke wangu amezimia usiku baada ya kutokwa na damu nyingi niliamua kumdanganya ili asije niomba PF3 na badaye niingie kwenye matatizo,nesi aliniomba hela ya matibabu lakini sikuwa na chochote kwa wakati ule lakini akanishauri nimwache mgonjwa pale ili mimi nirudi nyumbani nikatafute hela,ushauri ule ulikuwa mzuri hivyo niliamua kurudi nyumbani kwa haraka nilipofika nyumbani sikukawia nilimtafuta mtu wa kununua ng`ombe kwa sili sili ili mke mdogo asijue na cha kushukuru mipango ilienda vizuri nikauza ng`ombe mmoja  baada ya hapo nilirudi zahanati alipolazwa mke wangu ila nilipofika nesi alinipa maelezo mengine ambayo  nilikuwa sitegemei kuyasikia

Wewe kaka,mgonjwa uliyekuja naye usiku nilimfanyia vipimo vyote lakini hakuwa na tatizo lolote lakini kuna tatizo jingine pia

Kwa hiyo dada,yuko salama kabisa na tena tatizo gan?.kama hela nimekuja nazo nitakupa.

kaka hata sijui nikwelezaje yaani nilimwacha kwenye wodi akiwa mzima kabisa lakini sikumkuta na nimemtafuta lakini sijamwona

 unasemaje? Inamaana kaenda wapi sasa

Baada ya kuelezwa kuwa mke wangu mkubwa hayupo hospitalini pale,nilikaa kwenye mti mmoja pale zahanati kwa muda wa takribani saa moja na nusu   nikiwa natafakari nifanye kipi na niende wapi ikiwa mtu niliyekuja naye tena akiwa hana hata fahamu kabisa halafu naambiwa amepotea,sikuwa na chakufanya niliamua kurudi nyumbani na cha kushangaza zaidi nilipofika nyumbani  nilimkuta mke wangu mkubwa akiwa jikoni  anapika yaani mwanamke ambaye hakuwa na fahamu asubuhi na saa hizi saa saba anapika na je kafikaje huku? Hayo ni baadhi ya maswali yaliyokosa majibu niliyokuwa najiuliza na chakushangaza zaidi alikuwa mwenye furaha sana jambo hilo lilizidi kunichanganya zaidi

Mume wangu ulikuwa wapi tokea asubuhi sijakuona?

Niliwahi shambani

Niliongea huku sijui kipi chakufanya na nilipomshirikisha mke wangu mdogo kutokana na tukio lililotokea akanishauri niende kwa mganga wa kienyeji ambaye kila mara yeye huwa anaenda japo hajawahi hata kunishililisha juu ya mganga yule,mke wangu mdogo alinishauri tuzitumie zile hela nilizozipata kutokana na kuuza ng`ombe zilizokuwa za matibabu alinisihi twende tukampe mganga wa kienyeji ili atupe dawa ili  tuepuke mikosi na mimi nilikubali wazo lake maana lilikuwa wazo zuri nikaliunga mkono na utekelezaji wa safari ukaanza mara moja,baada ya chakula cha usiku wote tulienda kulala ila mimi na mke wangu tukaamka usiku kabisa mida ya saa 6 taratibu tukatoka nyumbani  ili mke mkubwa asijue chochote kwa bahati nzuri tulifika hadi kwa mganga salama na kwa bahati nzuri tena tukamkuta

Karibuni wote na leo sijalala kabisa maana nalijua tatizo lenu tokea jana na kama msingekuja leo mmoja wenu angekufa hasa wewe

Mimi? Sasa nimekosa nini

Huna kosa ila mkeo ambaye hazai ni mchawi na usiku wa jana umepambana na dudu likakupa nundu we unadhani ni mtu

 Tusaidie tunakuomba


Msaada wangu ni kuua tu,ukimwacha utakufa wewe

Mganga Yule alieleza mambo mengi sana akadai kuwa nilipomwacha mke wangu kule zahanati usiku wa jana hakuwa mke wangu ila alikuwa ni fisi na niliporudi nyumbani kutafuta hela ya matibababu alitoroka kichawi ,maelezo hayo yalinisikitisha na kuniogopesha sana ndipo mganga akanipa njia ili nijinusuru na mwanamke huyo,alinambia kuwa atamfanyia dawa mke wangu mkubwa apate hamu ya kwenda kwao na mimi nitekeleze mauaji hayo kwa mikono yangu wakati mke wangu mkubwa atakapokuwa anaenda kwao na nikishindwa kumuua mke wangu mkubwa ataniua siku siyo nyingi
Tulirudi nyumbani na kesho yake asubuhi mke wangu mkubwa alinifuata na  akaniomba ruhusa ili aende kwa wazazi wake kuwasalimia na mimi nikamkubalia ili maagizo ya mganga yatimie,nilimpa mashariti kuwa ataenda jioni siku ile ile ili nipate kutimiza maagizo ya mganga ya kumuua mke wangu mkubwa,ilipofika jioni mida ya saa 11 mke wangu mkubwa akaniaga na mimi nikamtakia safari njema,alipoondoka tu nyumbani nikachukua rungu,panga na kamba iliyosokotwa vizuri kwa nyuzi za katani,nikapita njia ya mkato ili  kumuwahi mke wangu kwenye msitu ambao uko karibu na njia ambayo mke wangu mara nyingi hupita akiwa anaenda kwao

Baada ya dakika kama 20 nilimwona mke wangu anakuja huku akiwa amebeba sanduku la nguo zake alikuwa anatembea kwa haraka hii ni kutokana na muda aliotoka nyumbani maana alitoka jioni sana hivyo alikuwa anataka kuwahi kufika alipokuwa anaenda, baada ya kumwona anakuja taratibu nikaanza kumnyatia na kabla hajashituka nilirusha rungu langu likampiga kisogoni palepale alianguka chini,nikamvuta kwenye majani ili niweze kumnyonga kwa kamba niliyokuwa nayo ili nitimize maagizo ya mganga kuwa lazima nimuue kwa kumnyonga kwa kamba ili kuficha ushahidi ili ionekane kuwa amejinyonga,nilitoa kamba iliyosokotwa kwa nyuzi za katani nikaangalia mti mzuri ili nikamnyonge kwa kamba niliyokuwa nayo…………….….INAENDELEA

       Tafadhali tembelea http://mla-ukoko.blogspot.com kwa mwendelezo wa hadithi pia share kwa marafiki

Comments

Popular posts from this blog

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA KWANZA (1)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA NNE(4)

HADITHI YA BABA MASUMBUKO SEHEMU YA TATU(3)